Amos 4:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sikilizeni neno hili, enyi wanawake ng'ombe wa Bashani mlioko huko mlimani Samaria; nyinyi mnaowaonea wanyonge, mnaowakandamiza maskini, na kuwaambia waume zenu: “Tuleteeni divai tunywe!” Sikilizeni ujumbe huu:
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sikilizeni neno hili, ninyi ng’ombe wa Bashani mlioko juu ya Mlima Samaria, ninyi wanawake mnaowadhulumu maskini, na kuwagandamiza wahitaji, na kuwaambia wanaume wenu, “Tuleteeni vinywaji!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lisikieni neno hili, enyi ng'ombe wa Bashani, mnaokaa juu ya mlima wa Samaria, mnaowaonea maskini, na kuwaponda wahitaji; mnaowaambia bwana zao, Haya! Leteni, tunywe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sikilizeni neno hili, enyi wanawake ng'ombe wa Bashani mlioko huko mlimani Samaria; nyinyi mnaowaonea wanyonge, mnaowakandamiza maskini, na kuwaambia waume zenu: “Tuleteeni divai tunywe!” Sikilizeni ujumbe huu:
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sikilizeni neno hili, ninyi ng'ombe wa Bashani mlioko juu ya Mlima Samaria, ninyi wanawake mnaowaonea maskini na kuwagandamiza wahitaji na kuwaambia wanaume wenu, “Tuleteeni vinywaji!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sikilizeni neno hili, ninyi ng’ombe wa Bashani mlioko juu ya Mlima Samaria, ninyi wanawake mnaowaonea maskini, na kuwagandamiza wahitaji, na kuwaambia wanaume wenu, “Tuleteeni vinywaji!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lisikieni neno hili, enyi ng'ombe wa Bashani, mnaokaa juu ya mlima wa Samaria, mnaowaonea maskini, na kuwaponda wahitaji; mnaowaambia bwana zao, Haya! Leteni, tunywe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sikilizeni neno hili, enyi wanawake ng'ombe wa Bashani mlioko huko mlimani Samaria; nyinyi mnaowaonea wanyonge, mnaowakandamiza maskini, na kuwaambia waume zenu: “Tuleteeni divai tunywe!” Sikilizeni ujumbe huu:
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lisikieni neno hili, ninyi ng'ombe wa Basani! Ninyi mlioko milimani kwa Samaria mkiwakorofisha wanyonge na kuwaponda maskini! Ninyi mnaowaambia bwana zao: Haya! Leteni, tunywe!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lisikieni neno hili, enyi ng’ombe wa Bashani, mnaokaa juu ya mlima wa Samaria, mnaowaonea maskini, na kuwaponda wahitaji; mnaowaambia bwana zao, Haya! Leteni, tunywe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musikilize neno hili, enyi wanawake munaokuwa kama ngombe wa Basani munaokuwa kule juu ya mulima wa Samaria. Ninyi munaowaonea wamasikini, munaowagandamiza wakosefu, na kuwaambia waume zenu: Mutuletee divai tukunywe! Musikilize ujumbe huu: