Amos 4:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Niliwaleteeni ugonjwa wa tauni kama ule nilioupelekea Misri. Niliwaua vijana wenu vitani, nikawachukua farasi wenu wa vita. Maiti zilijaa katika kambi zenu, uvundo wake ukajaa katika pua zenu. Hata hivyo hamkunirudia. Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Niliwapelekea tauni miongoni mwenu kama nilivyofanya kule Misri. Niliwaua vijana wenu wa kiume kwa upanga, na nikawachukua farasi wenu. Nilijaza pua zenu kwa uvundo kutoka kambi zenu, hata hivyo hamjanirudia mimi,” asema Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nimewapelekea tauni, kama tauni ya Misri; vijana wenu nimewaua kwa upanga, na farasi wenu nimewachukulia mbali; nami nimeupandisha uvundo wa matuo yenu na kuuingiza katika mianzi ya pua zenu; lakini hamkunirudia mimi, asema Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Niliwaleteeni ugonjwa wa tauni kama ule nilioupelekea Misri. Niliwaua vijana wenu vitani, nikawachukua farasi wenu wa vita. Maiti zilijaa katika kambi zenu, uvundo wake ukajaa katika pua zenu. Hata hivyo hamkunirudia. Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Niliwapelekea tauni miongoni mwenu kama nilivyofanya kule Misri. Niliwaua vijana wenu wa kiume kwa upanga, niliwachukua farasi wenu. Nilijaza pua zenu kwa uvundo kutoka kwenye kambi zenu, hata hivyo hamjanirudia mimi,” asema BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Niliwapelekea tauni miongoni mwenu kama nilivyofanya kule Misri. Niliwaua vijana wenu wa kiume kwa upanga, niliwachukua farasi wenu. Nilijaza pua zenu kwa uvundo kutoka kwenye kambi zenu, hata hivyo hamjanirudia mimi,” asema bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nimewaletea tauni, kama tauni ya Misri; vijana wenu nimewaua kwa upanga, na farasi wenu nimewachukulia mbali; nami nimeupandisha uvundo wa kambi zenu na kuuingiza katika mianzi ya pua zenu; lakini hamkunirudia mimi, asema BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Niliwaleteeni ugonjwa wa tauni kama ule nilioupelekea Misri. Niliwaua vijana wenu vitani, nikawachukua farasi wenu wa vita. Maiti zilijaa katika kambi zenu, uvundo wake ukajaa katika pua zenu. Hata hivyo hamkunirudia. Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nilituma kwenu magonjwa mabaya, kama nilivyovifanya huko Misri, nikawaua vijana wenu kwa panga, nao farasi wenu wakatekwa. Nikaupandisha mnuko mbaya wa kambi zenu, uingie puani mwenu, lakini hamkurudi kwangu; ndivyo, asemavyo Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nimewapelekea tauni, kama tauni ya Misri; vijana wenu nimewaua kwa upanga, na farasi wenu nimewachukulia mbali; nami nimeupandisha uvundo wa matuo yenu na kuuingiza katika mianzi ya pua zenu; lakini hamkunirudia mimi, asema BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Niliwaletea ugonjwa mukali kama ule nilioupelekea Misri. Niliwaua vijana wenu katika vita, nikatwaa farasi wenu wa vita. Maiti zilijaa katika kambi zenu, harufu yake mbaya ikajaa katika pua zenu. Hata hivyo hamukunirudilia. –Ni ujumbe wa Yawe.–