Amos 4:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mungu ndiye aliyeifanya milima, na kuumba upepo; ndiye amjulishaye mwanadamu mawazo yake; ndiye ageuzaye mchana kuwa usiku, na kukanyaga vilele vya dunia. Mwenyezi-Mungu wa Majeshi ndilo jina lake!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yeye ambaye hufanya milima, anaumba upepo, na kufunua mawazo yake kwa mwanadamu, yeye ageuzaye asubuhi kuwa giza, na kukanyaga mahali pa juu pa nchi: Bwana Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni ndilo jina lake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana, angalia, yeye aifanyizaye milima, na kuuumba upepo, na kumwambia mwanadamu mawazo yake, afanyaye asubuhi kuwa giza, na kupakanyaga mahali pa dunia palipoinuka; Bwana, Mungu wa majeshi, ndilo jina lake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mungu ndiye aliyeifanya milima, na kuumba upepo; ndiye amjulishaye mwanadamu mawazo yake; ndiye ageuzaye mchana kuwa usiku, na kukanyaga vilele vya dunia. Mwenyezi-Mungu wa Majeshi ndilo jina lake!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yeye ambaye hufanya milima, anaumba upepo, na kufunua mawazo yake kwa mwanadamu, yeye ageuzaye asubuhi kuwa giza, na kukanyaga mahali pa juu pa nchi: BWANA Mungu Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yeye ambaye hufanya milima, anaumba upepo, na kufunua mawazo yake kwa mwanadamu, yeye ageuzaye asubuhi kuwa giza, na kukanyaga mahali pa juu pa nchi: bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana, angalia, yeye aifanyaye milima, na kuumba upepo, na kumwambia mwanadamu mawazo yake, afanyaye asubuhi kuwa giza, na kupakanyaga mahali pa dunia palipoinuka; BWANA, Mungu wa majeshi, ndilo jina lake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mungu ndiye aliyeifanya milima, na kuumba upepo; ndiye amjulishaye mwanadamu mawazo yake; ndiye ageuzaye mchana kuwa usiku, na kukanyaga vilele vya dunia. Mwenyezi-Mungu wa Majeshi ndilo jina lake!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani utamwona atengenezaye milima, aumbaye upepo, amwambiaye mtu ayawazayo moyoni mwake, ni yeye ayageuzaye mapema kuwa giza akipita na kukanyaga juu ya vilima vya nchi; Bwana Mungu Mwenye vikosi ni Jina lake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana, angalia, yeye aifanyizaye milima, na kuuumba upepo, na kumwambia mwanadamu mawazo yake, afanyaye asubuhi kuwa giza, na kupakanyaga mahali pa dunia palipoinuka; BWANA, Mungu wa majeshi, ndilo jina lake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mungu ndiye aliyeifanya milima, na kuumba upepo; ndiye anayemujulisha mwanadamu mawazo yake; ndiye anayegeuza muchana kuwa usiku, na kukanyaga vilele vya dunia. Yawe wa majeshi ndilo jina lake!