Amos 4:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Toeni tambiko ya shukrani ya mikate iliyochachushwa. Tangazeni popote kwamba mmetoa kwa hiari; kwani ndivyo mnavyopenda kufanya! Mimi Bwana Mungu nimenena.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mchome mkate uliotiwa chachu kama sadaka ya shukrani, jisifuni kuhusu sadaka zenu za hiari: jigambeni kwa ajili ya sadaka hizo, enyi Waisraeli, kwa kuwa hili ndilo mnalopenda kulitenda,” asema Bwana Mungu Mwenyezi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
mkachome sadaka ya shukrani, ya kitu kilichotiwa chachu; mkatangaze sadaka mtoazo kwa hiari na kuzihubiri habari zake; kwa maana ndivyo viwapendezavyo ninyi, enyi wana wa Israeli, asema Bwana MUNGU.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Toeni tambiko ya shukrani ya mikate iliyochachushwa. Tangazeni popote kwamba mmetoa kwa hiari; kwani ndivyo mnavyopenda kufanya! Mimi Bwana Mungu nimenena.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mchome mkate uliotiwa chachu kama sadaka ya shukrani, jisifuni kuhusu sadaka zenu za hiari: jigambeni kwa ajili ya sadaka hizo, Enyi Waisraeli, kwa kuwa hili ndilo mnalopenda kulitenda,” asema BWANA Mwenyezi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mchome mkate uliotiwa chachu kama sadaka ya shukrani, jisifuni kuhusu sadaka zenu za hiari: jigambeni kwa ajili ya sadaka hizo, enyi Waisraeli, kwa kuwa hili ndilo mnalopenda kulitenda,” asema bwana Mwenyezi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
mkachome sadaka ya shukrani, ya kitu kilichotiwa chachu; mkatangaze sadaka mtoazo kwa hiari na kuzihubiri habari zake; kwa maana ndivyo viwapendezavyo ninyi, enyi wana wa Israeli, asema Bwana MUNGU.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Toeni tambiko ya shukrani ya mikate iliyochachushwa. Tangazeni popote kwamba mmetoa kwa hiari; kwani ndivyo mnavyopenda kufanya! Mimi Bwana Mungu nimenena.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Chomeni mikate yenye chachu, iwe shukrani! Tangazeni, visikilike, watu watoe vipaji viwapendezavyo! Kwani ndivyo, mnavyovipenda, ninyi wana wa Isiraeli; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
mkachome sadaka ya shukrani, ya kitu kilichotiwa chachu; mkatangaze sadaka mtoazo kwa hiari na kuzihubiri habari zake; kwa maana ndivyo viwapendezavyo ninyi, enyi wana wa Israeli, asema Bwana MUNGU.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutoe sadaka ya shukrani ya mikate isiyotiwa chachu. Mutangaze popote kwamba mumetoa kwa mapenzi; maana ndivyo munavyopenda kufanya! –Ni ujumbe wa Bwana wetu Yawe.–