Amos 4:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mimi niliwanyima chochote cha kutafuna, nikasababisha ukosefu wa chakula popote. Hata hivyo hamkunirudia. Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Niliwapa njaa kwenye kila mji, na ukosefu wa chakula katika kila mji, hata hivyo bado hamjanirudia mimi,” asema Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mimi nami nimewapa usafi wa meno katika miji yenu yote, na kutindikiwa na mkate mahali penu pote; lakini hamkunirudia mimi, asema Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mimi niliwanyima chochote cha kutafuna, nikasababisha ukosefu wa chakula popote. Hata hivyo hamkunirudia. Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Niliwapa njaa kwenye kila mji na ukosefu wa chakula katika kila mji, hata hivyo bado hamjanirudia mimi,” asema BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Niliwapa njaa kwenye kila mji, na ukosefu wa chakula katika kila mji, hata hivyo bado hamjanirudia mimi,” asema bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mimi nami nimewapa usafi wa meno katika miji yenu yote, na kutindikiwa na mkate mahali penu pote; lakini hamkunirudia mimi, asema BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mimi niliwanyima chochote cha kutafuna, nikasababisha ukosefu wa chakula popote. Hata hivyo hamkunirudia. Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nami niliwapa meno yakosayo kazi mijini mwenu mote nao ukosefu wa mkate pote, mnapokaa, lakini hamkurudi kwangu; ndivyo, asemavyo Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mimi nami nimewapa usafi wa meno katika miji yenu yote, na kutindikiwa na mkate mahali penu pote; lakini hamkunirudia mimi, asema BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mimi niliwanyima chochote cha kutafuna, nikasababisha ukosefu wa chakula popote. Hata hivyo hamukunirudilia. –Ni ujumbe wa Yawe.–