Amos 4:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Tena niliwanyima mvua miezi mitatu tu kabla ya mavuno. Niliunyeshea mvua mji mmoja, na mji mwingine nikaunyima. Shamba moja lilipata mvua, na lingine halikupata, likakauka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Pia niliwazuilia ninyi mvua miezi mitatu kabla ya kufikia mavuno. Nilinyesha mvua kwenye mji mmoja, lakini niliizuia mvua isinyeshe mji mwingine. Shamba moja lilipata mvua, na lingine halikupata, nalo likakauka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena nimeizuia mvua msiipate, ilipobaki miezi mitatu kabla ya mavuno; nami nimenyesha mvua juu ya mji mmoja, nikaizuia mvua isinyeshe juu ya mji mwingine; sehemu moja ilipata mvua, na sehemu isiyopata mvua ilikatika.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Tena niliwanyima mvua miezi mitatu tu kabla ya mavuno. Niliunyeshea mvua mji mmoja, na mji mwingine nikaunyima. Shamba moja lilipata mvua, na lingine halikupata, likakauka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Pia niliwazuilia ninyi mvua miezi mitatu kabla ya kufikia mavuno. Nilinyesha mvua kwenye mji mmoja, lakini niliizuia mvua isinyeshe mji mwingine. Shamba moja lilipata mvua, na lingine halikupata nalo likakauka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Pia niliwazuilia ninyi mvua miezi mitatu kabla ya kufikia mavuno. Nilinyesha mvua kwenye mji mmoja, lakini niliizuia mvua isinyeshe mji mwingine. Shamba moja lilipata mvua, na lingine halikupata, nalo likakauka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena nimeizuia mvua msiipate, ilipobaki miezi mitatu kabla ya mavuno; nami nimenyesha mvua juu ya mji mmoja, nikaizuia mvua isinyeshe juu ya mji mwingine; sehemu moja ilipata mvua, na sehemu isiyopata mvua ilikauka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Tena niliwanyima mvua miezi mitatu tu kabla ya mavuno. Niliunyeshea mvua mji mmoja, na mji mwingine nikaunyima. Shamba moja lilipata mvua, na lingine halikupata, likakauka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena mimi niliwanyima mvua, miezi mitatu tu ilipokuwa imesalia mpaka mavunoni, mji mmoja nikaunyeshea mvua, tena mwingine sikuunyeshea mvua, shamba moja likanyeshewa na mvua, jingine lisilopata mvua likakauka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena nimeizuia mvua msiipate, ilipobaki miezi mitatu kabla ya mavuno; nami nimenyesha mvua juu ya mji mmoja, nikaizuia mvua isinyeshe juu ya mji mwingine; sehemu moja ilipata mvua, na sehemu isiyopata mvua ilikatika.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tena niliwanyima mvua miezi mitatu tu mbele ya mavuno. Nilinyeshea mvua muji mumoja, na muji mwingine nikaunyima. Shamba moja lilipata mvua, na lingine halikupata, likakauka.