Amos 4:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wa miji miwili, mitatu wakakimbilia mji mwingine, wapate maji, lakini hayakuwatosha. Hata hivyo hamkunirudia. Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu walitangatanga mji hata mji kutafuta maji, lakini hawakupata ya kuwatosha kunywa, hata hivyo hamjanirudia mimi,” asema Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi kutoka miji miwili mitatu walitanga-tanga kuendea mji mwingine wapate kunywa maji, wasipate ya kuwatosha; lakini hamkunirudia mimi, asema Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wa miji miwili, mitatu wakakimbilia mji mwingine, wapate maji, lakini hayakuwatosha. Hata hivyo hamkunirudia. Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu walitangatanga mji hata mji kutafuta maji, lakini hawakupata ya kuwatosha kunywa, hata hivyo hamjanirudia mimi,” asema BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu walitangatanga mji hata mji kutafuta maji, lakini hawakupata ya kuwatosha kunywa, hata hivyo hamjanirudia mimi,” asema bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi kutoka miji miwili mitatu walitangatanga kuelekea mji mwingine wapate kunywa maji, wala hawakupata ya kuwatosha; lakini hamkunirudia mimi, asema BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wa miji miwili, mitatu wakakimbilia mji mwingine, wapate maji, lakini hayakuwatosha. Hata hivyo hamkunirudia. Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Miji miwili mitatu ikatangatanga kuendea mji mmoja tu, ndimo wapate kunywa maji, ijapo wasishibe, lakini hamkurudi kwangu; ndivyo, asemavyo Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi kutoka miji miwili mitatu walitanga-tanga kuendea mji mwingine wapate kunywa maji, wasipate ya kuwatosha; lakini hamkunirudia mimi, asema BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wa miji miwili au mitatu wakakimbilia katika muji mwingine, wapate maji, lakini hayakuwatoshelea. Hata hivyo hamukunirudilia. –Ni ujumbe wa Yawe.–