Amos 4:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Niliwapiga pigo la ukame na ukungu; nikakausha bustani na mashamba yenu ya mizabibu; nzige wakala mitini na mizeituni yenu. Hata hivyo hamkunirudia. Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mara nyingi nilizipiga bustani zenu na mashamba ya mizabibu, niliyapiga kwa kutu na ukungu. Nzige walitafuna tini zenu na miti ya mizeituni, hata hivyo hamjanirudia mimi,” asema Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nimewapiga kwa ukavu na koga; wingi wa bustani zenu na mashamba yenu ya mizabibu, na mitini yenu na mizeituni yenu imeliwa na tunutu; Lakini hamkunirudia mimi, asema Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Niliwapiga pigo la ukame na ukungu; nikakausha bustani na mashamba yenu ya mizabibu; nzige wakala mitini na mizeituni yenu. Hata hivyo hamkunirudia. Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mara nyingi nilizipiga bustani zenu na mashamba ya mizabibu, niliyapiga kwa kutu na ukungu. Nzige walitafuna tini zenu na miti ya mizeituni, hata hivyo hamjanirudia mimi,” asema BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mara nyingi nilizipiga bustani zenu na mashamba ya mizabibu, niliyapiga kwa kutu na ukungu. Nzige walitafuna tini zenu na miti ya mizeituni, hata hivyo hamjanirudia mimi,” asema bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nimewapiga kwa ukame na kuvu; wingi wa bustani zenu na mashamba yenu ya mizabibu, na mitini yenu na mizeituni yenu imeliwa na tunutu; Lakini hamkunirudia mimi, asema BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Niliwapiga pigo la ukame na ukungu; nikakausha bustani na mashamba yenu ya mizabibu; nzige wakala mitini na mizeituni yenu. Hata hivyo hamkunirudia. Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikawapiga ninyi, nikayaunguza mashamba na kuyakausha kabisa, tena mara nyingi nzige waliyala kwenu mashamba na mizabibu na mikuyu na michekele yenu, lakini hamkurudi kwangu; ndivyo, asemavyo Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nimewapiga kwa ukavu na koga; wingi wa bustani zenu na mashamba yenu ya mizabibu, na mitini yenu na mizeituni yenu imeliwa na tunutu; Lakini hamkunirudia mimi, asema BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Niliwapiga pigo la ukosefu wa maji na ukungu; nikakausha bustani na mashamba yenu ya mizabibu; nzige wakakula miti ya tini na mizeituni yenu. Hata hivyo hamukunirudilia. –Ni ujumbe wa Yawe.–