Amos 5:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana mimi najua wingi wa makosa yenu na ukubwa wa dhambi zenu; nyinyi mnawatesa watu wema, mnapokea rushwa na kuzuia fukara wasipate haki mahakamani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa ninajua hesabu ya makosa yenu na ukubwa wa dhambi zenu. Mmewadhulumu wenye haki na kupokea rushwa na kuzuia haki ya maskini mahakamani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana mimi najua jinsi maasi yenu yalivyo mengi, na jinsi dhambi zenu zilivyo kubwa; ninyi mnaowaonea wenye haki, mnaopokea rushwa, na kuwageuza wahitaji langoni wasipate haki yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana mimi najua wingi wa makosa yenu na ukubwa wa dhambi zenu; nyinyi mnawatesa watu wema, mnapokea rushwa na kuzuia fukara wasipate haki mahakamani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa ninajua hesabu ya makosa yenu na ukubwa wa dhambi zenu. Mmewaonea wenye haki na kupokea rushwa na kuzuia haki ya maskini mahakamani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa ninajua hesabu ya makosa yenu na ukubwa wa dhambi zenu. Mmewaonea wenye haki na kupokea rushwa na kuzuia haki ya maskini mahakamani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana mimi najua jinsi maasi yenu yalivyo mengi, na jinsi dhambi zenu zilivyo kubwa; ninyi mnaowaonea wenye haki, mnaopokea rushwa, na kuwageuza wahitaji langoni wasipate haki yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana mimi najua wingi wa makosa yenu na ukubwa wa dhambi zenu; nyinyi mnawatesa watu wema, mnapokea rushwa na kuzuia fukara wasipate haki mahakamani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani ninayajua mapotovu yenu yaliyo mengi nayo makosa yenu yanayozidi. Mnamsonga aliye mwongofu mkitaka kupenyezewa, mkawapotoa maskini, wasishinde shaurini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana mimi najua jinsi maasi yenu yalivyo mengi, na jinsi dhambi zenu zilivyo kubwa; ninyi mnaowaonea wenye haki, mnaopokea rushwa, na kuwageuza wahitaji langoni wasipate haki yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maana mimi ninajua wingi wa makosa yenu na ukubwa wa zambi zenu; ninyi munawatesa watu wema, munapokea kituliro na kuzuia wakosefu wasipate haki katika tribinali.