Amos 5:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Mwenyezi-Mungu, Mungu wa majeshi, naam, Mwenyezi-Mungu asema: “Patakuwa na kilio kila mahali mitaani; watu wataomboleza: ‘Ole! Ole!’ Wakulima wataitwa waje kuomboleza, na mabingwa wa kuomboleza waje kufanya matanga.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo hili ndilo Bwana, yeye Bwana Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, asemalo: “Kutakuwa na maombolezo barabarani zote, na vilio vya uchungu katika njia kuu zote. Wakulima wataitwa kuja kulia, na waombolezaji waje kuomboleza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa ajili ya hayo, asema Bwana, Mungu wa majeshi, aliye Bwana; Kutakuwako maombolezo katika njia kuu zote; nao watasema katika njia zote, Ole! Ole! Nao watamwita mkulima aje kuombolea, na hao walio hodari wa kulia waje kuomboleza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Mwenyezi-Mungu, Mungu wa majeshi, naam, Mwenyezi-Mungu asema: “Patakuwa na kilio kila mahali mitaani; watu wataomboleza: ‘Ole! Ole!’ Wakulima wataitwa waje kuomboleza, na mabingwa wa kuomboleza waje kufanya matanga.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo hili ndilo Bwana, BWANA Mungu Mwenye Nguvu Zote, asemalo: “Kutakuwepo maombolezo katika barabara zote na vilio vya uchungu mahali pa njia kuu. Wakulima wataitwa kuja kulia na waombolezaji waje kuomboleza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo hili ndilo Bwana, bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, asemalo: “Kutakuwepo maombolezo katika barabara zote na vilio vya uchungu katika njia kuu zote. Wakulima wataitwa kuja kulia, na waombolezaji waje kuomboleza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa ajili ya hayo, asema BWANA, Mungu wa majeshi, aliye Bwana; Kutakuwako maomboleza katika njia kuu zote; nao watasema katika njia zote, Ole! Ole! Nao watamwita mkulima aje kuombolea, na hao walio hodari wa kulia waje kuomboleza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Mwenyezi-Mungu, Mungu wa majeshi, naam, Mwenyezi-Mungu asema: “Patakuwa na kilio kila mahali mitaani; watu wataomboleza: ‘Ole! Ole!’ Wakulima wataitwa waje kuomboleza, na mabingwa wa kuomboleza waje kufanya matanga.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kweli Bwana Mungu Mwenye vikosi, yeye Bwana anasema hivi: Katika viwanja vyote yatakuwako maombolezo, napo barabarani po pote watalia kwamba: Hoi! Hoi! Mkulima watamwita shambani, aje kuingia matanga, nao wajuao maombolezo watawaita, waje kuwalilia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa ajili ya hayo, asema BWANA, Mungu wa majeshi, aliye Bwana; Kutakuwako maombolezo katika njia kuu zote; nao watasema katika njia zote, Ole! Ole! Nao watamwita mkulima aje kuombolea, na hao walio hodari wa kulia waje kuomboleza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Yawe, Mungu wa majeshi, Bwana wetu anasema hivi: Kutakuwa kilio kila nafasi katika barabara za muji; watu wataomboleza: Ole! Ole! Walimaji wataitwa kuja kuomboleza, na wafundi wa kuomboleza kuja kufanya kilio.