Amos 5:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mambo yatakuwa kama mtu aliyekimbia simba, halafu akakumbana na dubu! Au kama mtu anayerudi nyumbani kwake, akatia mkono ukutani, akaumwa na nyoka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Itakuwa kama vile mtu aliyemkimbia simba kumbe akakutana na dubu, kama vile mtu aliyeingia nyumbani mwake na kuupumzisha mkono wake kwenye ukuta, kumbe akaumwa na nyoka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ni kama mtu aliyemkimbia simba, akakutana na dubu; au aliingia katika nyumba akauegemeza mkono wake ukutani, nyoka akamwuma.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mambo yatakuwa kama mtu aliyekimbia simba, halafu akakumbana na dubu! Au kama mtu anayerudi nyumbani kwake, akatia mkono ukutani, akaumwa na nyoka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Itakuwa kama vile mtu aliyemkimbia simba kumbe akakutana na dubu, kama vile mtu aliyeingia nyumbani mwake na kuupumzisha mkono wake kwenye ukuta kumbe akaumwa na nyoka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Itakuwa kama vile mtu aliyemkimbia simba kumbe akakutana na dubu, kama vile mtu aliyeingia nyumbani mwake na kuupumzisha mkono wake kwenye ukuta, kumbe akaumwa na nyoka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ni kama mtu aliyemkimbia simba, akakutana na dubu; au aliingia katika nyumba akauegemeza mkono wake ukutani, nyoka akamwuma.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mambo yatakuwa kama mtu aliyekimbia simba, halafu akakumbana na dubu! Au kama mtu anayerudi nyumbani kwake, akatia mkono ukutani, akaumwa na nyoka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Itakuwa, kama mtu akimkimbia simba, akaja kukutana na chui, au kama mtu akiingia nyumbani, akauegemeza mkono wake ukutani, kisha akatokea nyoka, akamwuma.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ni kama mtu aliyemkimbia simba, akakutana na dubu; au aliingia katika nyumba akauegemeza mkono wake ukutani, nyoka akamwuma.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mambo yatakuwa kama mutu aliyekimbia simba, halafu anakutana na dubu! Au kama mutu anayerudi kwa nyumba yake, na kutia mukono wake kwenye ukuta, na kuumwa na nyoka.