Amos 5:26 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Je, wakati huo mlibeba kama sasa vinyago vya mungu wenu Sakuthi mfalme wenu na vinyago vya Kaiwani mungu wenu wa nyota, vitu ambavyo mlijitengenezea wenyewe?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mmeyainua madhabahu ya Sikuthi mungu wenu mtawala, na Kiuni mungu wenu wa nyota, ambao mliwatengeneza wenyewe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naam, mtamchukua Sikuthi, mfalme wenu, na Kiuni, sanamu zenu, nyota ya mungu wenu, mliojifanyizia wenyewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Je, wakati huo mlibeba kama sasa vinyago vya mungu wenu Sakuthi mfalme wenu na vinyago vya Kaiwani mungu wenu wa nyota, vitu ambavyo mlijitengenezea wenyewe?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mmeyainua madhabahu ya mfalme wenu: Sikuthi mungu wenu mtawala, Kiuni mungu wenu wa nyota; ambao mliwatengeneza wenyewe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mmeyainua madhabahu ya mfalme wenu, Sikuthi mungu wenu mtawala, na Kiuni mungu wenu wa nyota, ambao mliwatengeneza wenyewe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naam, mtamchukua Sikuthi, mfalme wenu, na Kiuni, sanamu zenu, nyota ya mungu wenu, mliojifanyia wenyewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Je, wakati huo mlibeba kama sasa vinyago vya mungu wenu Sakuthi mfalme wenu na vinyago vya Kaiwani mungu wenu wa nyota, vitu ambavyo mlijitengenezea wenyewe?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa kuwa mlimchukua Sikuti, awe mfalme wenu, navyo vinyua vyenu vya Kiyuni, mlivyojifanyizia wenyewe, viwe nyota zake mungu wenu:
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naam, mtamchukua Sikuthi, mfalme wenu, na Kiuni, sanamu zenu, nyota ya mungu wenu, mliojifanyizia wenyewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mulibeba kama vile sasa sanamu za mungu wenu Sakuti mufalme wenu na sanamu za Kiuni mungu wenu wa nyota, vitu ambavyo mulijitengenezea wenyewe?