Amos 5:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana Bwana Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Watu 1,000 watatoka mjini kwenda kupigana lakini watarejea 100 tu; wataondoka watu 100 wa kijiji kimoja lakini watanusurika watu kumi tu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: “Mmoja wa miji yako utakapopeleka watu elfu moja vitani kwa ajili ya Israeli, mia moja tu watarudi; wakati mji utakapopeleka mia moja, kumi tu ndio watarudi hai.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuwa Bwana MUNGU asema hivi; Mji uliotoka nje wenye watu elfu, utasaziwa watu mia, na mji uliotoka wenye watu mia, utasaziwa watu kumi, kwa nyumba ya Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana Bwana Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Watu 1,000 watatoka mjini kwenda kupigana lakini watarejea 100 tu; wataondoka watu 100 wa kijiji kimoja lakini watanusurika watu kumi tu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: “Wakati mmoja wa miji yako utakapopeleka watu elfu moja vitani, mia moja tu watarudi; wakati mji utakapopeleka mia moja, kumi tu ndio watarudi hai.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo: “Wakati mmoja wa miji yako utakapopeleka watu elfu moja vitani kwa ajili ya Israeli, mia moja tu watarudi; wakati mji utakapopeleka mia moja, kumi tu ndio watarudi hai.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuwa Bwana MUNGU asema hivi; Mji uliotoka nje wenye watu elfu moja, utabakiziwa watu mia moja, na mji uliotoka wenye watu mia moja, utabakiziwa watu kumi, kwa nyumba ya Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana Bwana Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Watu 1,000 watatoka mjini kwenda kupigana lakini watarejea 100 tu; wataondoka watu 100 wa kijiji kimoja lakini watanusurika watu kumi tu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Mji unaopeleka elfu vitani utasaza mia tu, nao unaopeleka mia utasaza kumi tu kwao walio mlango wa Isiraeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kuwa Bwana MUNGU asema hivi; Mji uliotoka nje wenye watu elfu, utasaziwa watu mia, na mji uliotoka wenye watu mia, utasaziwa watu kumi, kwa nyumba ya Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maana Bwana wetu Yawe anasema: Itakuwa hivi: juu yenu ninyi Waisraeli: Watu elfu moja wanatoka katika muji kwenda kupigana lakini watarudia watu mia moja tu; wataondoka watu mia moja wa kijiji kimoja lakini watu kumi tu wataponyoka.