Amos 5:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huyo aliyezifanya Kilimia na sayari Orioni, ambaye huligeuza giza nene kuwa mchana, na mchana kuwa usiku; yeye ambaye ayaitaye pamoja maji ya bahari na kuyamwaga juu ya nchi kavu, Mwenyezi-Mungu ndilo jina lake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
(yeye ambaye alifanya Kilimia na Orioni, ambaye hugeuza giza kuwa mapambazuko na mchana kuwa usiku, ambaye huyaita maji ya bahari na kuyamwaga juu ya nchi: Mwenyezi Mungu ndilo jina lake;
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
mtafuteni yeye afanyaye Kilimia na Orioni, na kukigeuza kivuli cha mauti kuwa asubuhi, na kuufanya mchana kuwa giza kwa usiku; yeye ayaitaye maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya uso wa nchi; Bwana, ndilo jina lake;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Huyo aliyezifanya Kilimia na sayari Orioni, ambaye huligeuza giza nene kuwa mchana, na mchana kuwa usiku; yeye ambaye ayaitaye pamoja maji ya bahari na kuyamwaga juu ya nchi kavu, Mwenyezi-Mungu ndilo jina lake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
(yeye ambaye alifanya Kilimia na Orioni, ambaye hugeuza giza kuwa mapambazuko na mchana kuwa usiku, ambaye huyaita maji ya bahari na kuyamwaga juu ya uso wa nchi: BWANA ndilo jina lake;
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
(yeye ambaye alifanya Kilimia na Orioni, ambaye hugeuza giza kuwa mapambazuko na mchana kuwa usiku, ambaye huyaita maji ya bahari na kuyamwaga juu ya uso wa nchi: bwana ndilo jina lake;
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
mtafuteni yeye afanyaye Kilimia na Orioni, na kukigeuza kivuli cha mauti kuwa asubuhi, na kuufanya mchana kuwa giza usiku; yeye ayaitaye maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya uso wa nchi; BWANA, ndilo jina lake;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Huyo aliyezifanya Kilimia na sayari Orioni, ambaye huligeuza giza nene kuwa mchana, na mchana kuwa usiku; yeye ambaye ayaitaye pamoja maji ya bahari na kuyamwaga juu ya nchi kavu, Mwenyezi-Mungu ndilo jina lake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yeye ndiye aliyezifanya nyota, zile za Kilimia nazo zake Choma, nikuchome! Yeye ndiye anayeigeuza giza kuwa mapema, tena mwanga wa mchana huugeuza kuwa giza ya usiku! Yeye ndiye anayeyaita maji ya bahari, akayafurikisha juu ya nchi! Bwana ni Jina lake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
mtafuteni yeye afanyaye Kilimia na Orioni, na kukigeuza kivuli cha mauti kuwa asubuhi, na kuufanya mchana kuwa giza kwa usiku; yeye ayaitaye maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya uso wa nchi; BWANA, ndilo jina lake;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Huyo aliyezifanya nyota zinazoitwa Kilimia na Orioni, ambaye analigeuza giza nene kuwa muchana, na muchana kuwa usiku; yeye anayekusanya maji ya bahari na kuyamwanga juu ya inchi kavu, Yawe ndilo jina lake.