Amos 6:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Na atakapokuja mjomba wa aliyekufa kuitoa maiti nje aichome, akamwuliza yeyote atakayekuwako ndani pembeni mwa nyumba, “Je kuna mtu mwingine pamoja nawe?” Naye atamjibu, “La! Hamna!” Naye atamwambia, “Nyamaza kimya! Tusilitaje hata jina la Mwenyezi-Mungu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama jamaa ambaye atachoma miili akija ili kuitoa nje ya nyumba, na kumuuliza yeyote ambaye bado anajificha humo, “Je, yuko mtu yeyote pamoja nawe?” Naye akisema, “Hapana,” ndipo atakaposema, “Nyamaza! Haturuhusiwi kutaja jina la Mwenyezi Mungu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mjomba wa mtu atakapomwinua, yaani, yeye amchomaye moto, ili atoe mifupa yake nyumbani, naye atakapomwambia yeye aliye katika pande za ndani za nyumba, Je! Yuko mtu ye yote pamoja nawe? Naye atakaposema, La, hapana; ndipo atasema, Nyamaza kimya; maana hatuna ruhusa kulitaja jina la Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Na atakapokuja mjomba wa aliyekufa kuitoa maiti nje aichome, akamwuliza yeyote atakayekuwako ndani pembeni mwa nyumba, “Je kuna mtu mwingine pamoja nawe?” Naye atamjibu, “La! Hamna!” Naye atamwambia, “Nyamaza kimya! Tusilitaje hata jina la Mwenyezi-Mungu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama jamaa ambaye atachoma miili akija ili kuitoa nje ya nyumba, na kumwuliza ye yote ambaye bado anajificha humo, “Je, yuko mtu ye yote pamoja nawe?” Naye akisema, “Hapana,” ndipo atakaposema, “Nyamaza kimya! Haturuhusiwi kutaja jina la BWANA.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama jamaa ambaye atachoma miili akija ili kuitoa nje ya nyumba, na kumuuliza yeyote ambaye bado anajificha humo, “Je, yuko mtu yeyote pamoja nawe?” Naye akisema, “Hapana,” ndipo atakaposema, “Nyamaza kimya! Haturuhusiwi kutaja jina la bwana.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mjomba wa mtu atakapomwinua, yaani, yeye amchomaye moto, ili atoe mifupa yake nyumbani, naye atakapomwambia yeye aliye katika pande za ndani za nyumba, Je! Yuko mtu yeyote pamoja nawe? Naye atakaposema, La, hapana; ndipo atasema, Nyamaza kimya; maana hatuna ruhusa kulitaja jina la BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Na atakapokuja mjomba wa aliyekufa kuitoa maiti nje aichome, akamwuliza yeyote atakayekuwako ndani pembeni mwa nyumba, “Je kuna mtu mwingine pamoja nawe?” Naye atamjibu, “La! Hamna!” Naye atamwambia, “Nyamaza kimya! Tusilitaje hata jina la Mwenyezi-Mungu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndugu ya mtu apaswaye na kumteketeza mwenziwe akimchukua, aitoe mifupa yake nyumbani, kama anamwuliza aliomo nyumbani ndani: Yumo, uliye naye humu? atamjibu: Wamekwisha kufa! Ndipo, atakapomwambia: Nyamaza kimya! Kwani haifai kulikumbusha Jina la Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mjomba wa mtu atakapomwinua, yaani, yeye amchomaye moto, ili atoe mifupa yake nyumbani, naye atakapomwambia yeye aliye katika pande za ndani za nyumba, Je! Yuko mtu ye yote pamoja nawe? Naye atakaposema, La, hapana; ndipo atasema, Nyamaza kimya; maana hatuna ruhusa kulitaja jina la BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na mujomba wa yule aliyekufa atakapokuja kuitoa maiti inje aichome, akimwuliza yeyote atakayekuwa ndani pembeni ya nyumba: Kuna mutu mwingine pamoja nawe? Atajibiwa: Hakuna! Naye atamwambia: Nyamaza kimya! Tusilitaje hata jina la Yawe.