Amos 6:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tazama! Mwenyezi-Mungu anatoa amri, nalo jumba kubwa labomoka vipandevipande, na nyumba ndogo kusagikasagika.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ameamuru, naye atabomoa jumba kubwa vipande vipande na nyumba ndogo vipande vidogo vidogo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana, angalia, Bwana atoa amri, na nyumba kubwa itapigwa na kuwa na mahali palipobomolewa, na nyumba ndogo nayo itapigwa iwe na nyufa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tazama! Mwenyezi-Mungu anatoa amri, nalo jumba kubwa labomoka vipandevipande, na nyumba ndogo kusagikasagika.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa BWANA ameamuru, naye atabomoa jumba kubwa vipande vipande na nyumba ndogo vipande vidogo vidogo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa bwana ameamuru, naye atabomoa jumba kubwa vipande vipande na nyumba ndogo vipande vidogo vidogo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana, angalia, BWANA atoa amri, na jumba kuu litabomolewa vipande vipande, na nyumba ndogo kuwa vigae.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tazama! Mwenyezi-Mungu anatoa amri, nalo jumba kubwa labomoka vipandevipande, na nyumba ndogo kusagikasagika.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani mtaona: Bwana akiagiza, ndipo, watakapozipiga nyumba kubwa, hata zibomoke, nazo nyumba ndogo, hata ziatuke nyufa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana, angalia, BWANA atoa amri, na nyumba kubwa itapigwa na kuwa na mahali palipobomolewa, na nyumba ndogo nayo itapigwa iwe na nyufa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe anatoa amri, na nyumba kubwa inabomoka vipandevipande, na nyumba ndogo kusagikasagika.