Amos 6:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Haya! Nendeni Kalne mkaangalie kila mahali, tokeni huko mwende hadi mji ule mkubwa wa Hamathi, kisha teremkeni hadi Gathi kwa Wafilisti. Je, falme zao si bora kuliko zenu na eneo lao si bora kuliko lenu?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nendeni Kalne mkaone kutoka huko; mwende hadi Hamathi iliyo kuu, kisha mshuke hadi Gathi ya Wafilisti. Je, wao ni bora kuliko falme zenu mbili? Je, nchi yao ni kubwa kuliko yenu?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Piteni hata Kalne, mkaone; tena tokea huko enendeni hata Hamathi iliyo kuu; kisha shukeni hata Gathi ya Wafilisti; je! Ninyi ni bora kuliko falme hizi? Au mpaka wao ni mkubwa kuliko mpaka wenu?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Haya! Nendeni Kalne mkaangalie kila mahali, tokeni huko mwende hadi mji ule mkubwa wa Hamathi, kisha teremkeni hadi Gathi kwa Wafilisti. Je, falme zao si bora kuliko zenu na eneo lao si bora kuliko lenu?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nendeni Kalne mkaone kutoka huko; mwende hadi Hamathi iliyo kuu, kisha mshuke hadi Gathi ya Wafilisti. Je, wao ni bora kuliko falme zenu mbili? Je, nchi yao ni kubwa kuliko yenu?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nendeni Kalne mkaone kutoka huko; mwende hadi Hamathi iliyo kuu, kisha mshuke hadi Gathi ya Wafilisti. Je, wao ni bora kuliko falme zenu mbili? Je, nchi yao ni kubwa kuliko yenu?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Piteni hadi Kalne, mkaone; tena tokea huko nendeni hadi Hamathi iliyo kuu; kisha shukeni hadi Gathi ya Wafilisti; je! Ninyi ni bora kuliko falme hizi? Au eneo lao ni kubwa kuliko eneo lenu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Haya! Nendeni Kalne mkaangalie kila mahali, tokeni huko mwende hadi mji ule mkubwa wa Hamathi, kisha teremkeni hadi Gathi kwa Wafilisti. Je, falme zao si bora kuliko zenu na eneo lao si bora kuliko lenu?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Haya! Nendeni Kalne, mkatazame! Tena tokeni huko kwenda Hamati ulio mji mkuu! Kisha shukeni Gati kwa Wafilisti, mwone! Je? Ninyi m wema kuliko watu wa nchi hizo za kifalme? Je? Mipaka yao siyo mikubwa kuliko mipaka yenu?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Piteni hata Kalne, mkaone; tena tokea huko enendeni hata Hamathi iliyo kuu; kisha shukeni hata Gathi ya Wafilisti; je! Ninyi ni bora kuliko falme hizi? Au mpaka wao ni mkubwa kuliko mpaka wenu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muende Kalne, muangalie. Tokea kule muende mpaka katika ule muji mukubwa wa Hamati, kisha mutelemuke mpaka Gati kwa Wafilistini. Mutatambua kwamba ninyi si bora kuliko falme zile, hata kama eneo lao ni ndogo zaidi ya lenu.