Amos 6:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Bwana Mwenyezi-Mungu ameapa kwa nafsi yake; Mwenyezi-Mungu, Mungu wa majeshi asema: “Nachukizwa mno na kiburi cha wazawa wa Yakobo; tena nayachukia majumba yao ya fahari. Mji wao na vyote vilivyomo nitawapa adui zao.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Bwana Mungu Mwenyezi ameapa kwa nafsi yake mwenyewe: Bwana Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, asema: “Nachukia kiburi cha Yakobo, nachukia ngome zake; nitautoa mji wao na kila kitu kilicho ndani yake.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana MUNGU ameapa kwa nafsi yake, asema Bwana, Mungu wa majeshi; Naizira fahari ya Yakobo, nachukizwa na majumba yake; kwa sababu hiyo nitautoa huo mji, pamoja na wote waliomo ndani yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Bwana Mwenyezi-Mungu ameapa kwa nafsi yake; Mwenyezi-Mungu, Mungu wa majeshi asema: “Nachukizwa mno na kiburi cha wazawa wa Yakobo; tena nayachukia majumba yao ya fahari. Mji wao na vyote vilivyomo nitawapa adui zao.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA Mwenyezi ameapa kwa nafsi yake mwenyewe: BWANA Mungu Mwenye Nguvu Zote asema: “Nachukia kiburi cha Yakobo, nachukia ngome zake; nitautoa mji wao na kila kitu kilichomo ndani mwake.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana Mwenyezi ameapa kwa nafsi yake mwenyewe: bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote asema: “Nachukia kiburi cha Yakobo, nachukia ngome zake; nitautoa mji wao na kila kitu kilichomo ndani mwake.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Bwana MUNGU ameapa kwa nafsi yake, asema BWANA, Mungu wa majeshi; Naizira fahari ya Yakobo, nachukizwa na majumba yake; kwa sababu hiyo nitautoa huo mji, pamoja na wote waliomo ndani yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Bwana Mwenyezi-Mungu ameapa kwa nafsi yake; Mwenyezi-Mungu, Mungu wa majeshi asema: “Nachukizwa mno na kiburi cha wazawa wa Yakobo; tena nayachukia majumba yao ya fahari. Mji wao na vyote vilivyomo nitawapa adui zao.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, asemavyo Bwana Mungu Mwenye vikosi: Bwana Mungu ameapa rohoni mwake kwamba: Majivuno ya Yakobo hunitapisha, nikachukizwa na majumba yake, kwa sababu hii nitautoa huo mji pamoja nayo yote yaliyomo mwake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Bwana MUNGU ameapa kwa nafsi yake, asema BWANA, Mungu wa majeshi; Naizira fahari ya Yakobo, nachukizwa na majumba yake; kwa sababu hiyo nitautoa huo mji, pamoja na wote waliomo ndani yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Bwana wetu Yawe ameapa kwa nafsi yake: Ninachukizwa sana na kiburi cha wazao wa Yakobo; tena ninachukia nyumba zao nzuri sana. –Ni ujumbe wa Yawe.– Muji wao na vyote vinavyokuwa ndani yake nitavipatia waadui zake.