Amos 7:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo, Mwenyezi-Mungu asema hivi: ‘Mkeo atakuwa malaya mjini, na wanao wa kiume na kike watauawa vitani. Ardhi yako itagawanywa na kupewa wengine, nawe binafsi utafia katika nchi najisi, nao Waisraeli hakika watapelekwa uhamishoni, mbali kabisa na nchi yao.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kwa hiyo hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “ ‘Mke wako atakuwa kahaba mjini, nao wana wako wa kiume na wa kike watauawa kwa upanga. Shamba lako litapimwa na kugawanywa, na wewe mwenyewe utafia katika nchi ya kipagani. Nayo Israeli kwa hakika itaenda uhamishoni, mbali na nchi yao.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kwa hiyo, Bwana asema hivi, Mke wako atakuwa kahaba mjini, na wana wako na binti zako wataanguka kwa upanga, na shamba lako litagawanywa kwa kamba; na wewe mwenyewe utakufa katika nchi iliyo najisi; na bila shaka Israeli atachukuliwa mbali hali ya kufungwa kutoka nchi yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo, Mwenyezi-Mungu asema hivi: ‘Mkeo atakuwa malaya mjini, na wanao wa kiume na kike watauawa vitani. Ardhi yako itagawanywa na kupewa wengine, nawe binafsi utafia katika nchi najisi, nao Waisraeli hakika watapelekwa uhamishoni, mbali kabisa na nchi yao.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kwa hiyo hili ndilo asemalo BWANA: “ ‘Mke wako atakuwa kahaba mjini, nao wana wako na binti zako watauawa kwa upanga. Shamba lako litapimwa na kugawanywa, na wewe mwenyewe utafia katika nchi ya kipagani. Nayo Israeli kwa hakika itakwenda uhamishoni, mbali na nchi yao.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kwa hiyo hili ndilo asemalo bwana: “ ‘Mke wako atakuwa kahaba mjini, nao wana wako na binti zako watauawa kwa upanga. Shamba lako litapimwa na kugawanywa, na wewe mwenyewe utafia katika nchi ya kipagani. Nayo Israeli kwa hakika itakwenda uhamishoni, mbali na nchi yao.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kwa hiyo, BWANA asema hivi, Mke wako atakuwa kahaba mjini, na wana wako na binti zako wataanguka kwa upanga, na shamba lako litagawanywa kwa kamba; na wewe mwenyewe utakufa katika nchi iliyo najisi; na bila shaka Israeli atapelekwa uhamishoni mbali na nchi yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo, Mwenyezi-Mungu asema hivi: ‘Mkeo atakuwa malaya mjini, na wanao wa kiume na kike watauawa vitani. Ardhi yako itagawanywa na kupewa wengine, nawe binafsi utafia katika nchi najisi, nao Waisraeli hakika watapelekwa uhamishoni, mbali kabisa na nchi yao.’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ni kwa sababu hii, Bwana akisema hivyo: Mkeo atakuwa mgoni humu mjini, nao wanao wa kiume na wa kike watauawa kwa upanga, nalo fungu lako la nchi litagawanywa kwa kupimwa na kamba. Nawe wewe utakufa katika nchi iliyo na mwiko wa kuikaa, nao Waisiraeli watatekwa na kuhamishwa, watoke katika nchi yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kwa hiyo, BWANA asema hivi, Mke wako atakuwa kahaba mjini, na wana wako na binti zako wataanguka kwa upanga, na shamba lako litagawanywa kwa kamba; na wewe mwenyewe utakufa katika nchi iliyo najisi; na bila shaka Israeli atachukuliwa mbali hali ya kufungwa kutoka nchi yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo, Yawe anasema hivi: Muke wako atakuwa kahaba katika muji, na wana wako na wabinti zako watauawa katika vita. Inchi yako itagawanywa na kupewa wengine, nawe mwenyewe utakufia katika inchi inayohesabiwa kuwa chafu; nao Waisraeli hakika watapelekwa katika uhamisho, mbali kabisa na inchi yao.