Amos 7:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Niliwaona nzige hao wakila na kumaliza kila jani katika nchi. Ndipo nikasema: “Ee Bwana Mwenyezi-Mungu, nakusihi utuhurumie! Wazawa wa Yakobo watawezaje kuishi? Wao ni wadogo mno!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati nzige walikuwa wamekula mimea yote ya nchi, nililia kwa sauti kuu, “Bwana Mungu Mwenyezi, samehe! Je, Yakobo atawezaje kuendelea kuishi? Yeye ni mdogo sana!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa, nzige walipokwisha kula majani ya nchi, ndipo nikasema, Ee Bwana MUNGU, samehe, nakusihi; Yakobo atasimamaje? Kwa maana ni mdogo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Niliwaona nzige hao wakila na kumaliza kila jani katika nchi. Ndipo nikasema: “Ee Bwana Mwenyezi-Mungu, nakusihi utuhurumie! Wazawa wa Yakobo watawezaje kuishi? Wao ni wadogo mno!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati nzige walipokuwa wamekula mimea yote ya nchi, nililia kwa sauti kuu, “BWANA Mwenyezi, samehe! Je, Yakobo atawezaje kuendelea kuishi? Yeye ni mdogo sana!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati nzige walikuwa wamekula mimea yote ya nchi, nililia kwa sauti kuu, “ bwana Mwenyezi, samehe! Je, Yakobo atawezaje kuendelea kuishi? Yeye ni mdogo sana!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa, nzige walipokwisha kula majani ya nchi, ndipo nikasema, Ee Bwana MUNGU, samehe, nakusihi; Yakobo atasimamaje? Kwa maana ni mdogo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Niliwaona nzige hao wakila na kumaliza kila jani katika nchi. Ndipo nikasema: “Ee Bwana Mwenyezi-Mungu, nakusihi utuhurumie! Wazawa wa Yakobo watawezaje kuishi? Wao ni wadogo mno!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa, nzige walipokwisha kula majani ya nchi, nikasema: Bwana Mungu, waachilie! Yakobo atawezaje kusimama? Kwani yeye ni mdogo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa, nzige walipokwisha kula majani ya nchi, ndipo nikasema, Ee Bwana MUNGU, samehe, nakusihi; Yakobo atasimamaje? Kwa maana ni mdogo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Niliwaona nzige hao wakikula na kumaliza kila jani katika inchi. Halafu nikasema: Ee Bwana wetu Yawe, ninakusihi utuhurumie! Wazao wa Yakobo wataweza kuishi namna gani? Wao ni wadogo sana!