Amos 7:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Bwana Mwenyezi-Mungu akabadili nia yake, akasema, “Haitakuwa hivyo!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo Mwenyezi Mungu akaghairi. Kisha Mwenyezi Mungu akasema, “Hili halitatokea.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana akaghairi katika jambo hili. Jambo hili halitakuwa, asema Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Bwana Mwenyezi-Mungu akabadili nia yake, akasema, “Haitakuwa hivyo!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo BWANA akaghairi. Kisha BWANA akasema, “Hili halitatokea.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo bwana akaghairi. Kisha bwana akasema, “Hili halitatokea.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA akaghairi katika jambo hili. Jambo hili halitakuwa, asema BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Bwana Mwenyezi-Mungu akabadili nia yake, akasema, “Haitakuwa hivyo!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Bwana Mungu alipoigeuza roho kwa ajili ya hayo naye Bwana akasema: Hayatakuwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA akaghairi katika jambo hili. Jambo hili halitakuwa, asema BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Bwana wetu Yawe akabadilisha nia yake, akasema: Halitatukia!