Amos 7:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Bwana Mwenyezi-Mungu alinijalia maono mengine: Nilimwona Bwana Mwenyezi-Mungu akiuita moto wa hukumu ya kuwaadhibu watu. Moto huo uliunguza vilindi vikuu vya bahari, ukaanza kuiteketeza nchi kavu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hili ndilo Bwana Mungu Mwenyezi alilonionesha katika maono: Bwana Mungu Mwenyezi alikuwa akiita hukumu ya moto; nao ulikausha vilindi vikuu, ukateketeza nchi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Haya ndiyo aliyonionyesha Bwana MUNGU; tazama, Bwana MUNGU aliita ili kushindana kwa moto; nao ukavila vilindi vikuu, ukataka kuiteketeza nchi kavu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Bwana Mwenyezi-Mungu alinijalia maono mengine: Nilimwona Bwana Mwenyezi-Mungu akiuita moto wa hukumu ya kuwaadhibu watu. Moto huo uliunguza vilindi vikuu vya bahari, ukaanza kuiteketeza nchi kavu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hili ndilo BWANA Mwenyezi alilonionyesha katika maono: BWANA Mwenyezi alikuwa akiita hukumu ya moto; nao ulikausha vilindi vikuu, ukateketeza nchi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hili ndilo bwana Mwenyezi alilonionyesha katika maono: bwana Mwenyezi alikuwa akiita hukumu ya moto; nao ulikausha vilindi vikuu, ukateketeza nchi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Haya ndiyo aliyonionesha Bwana MUNGU; tazama, Bwana MUNGU aliita ili kushindana kwa moto; nao ukaviteketeza vilindi vikuu, ukataka kuiteketeza nchi kavu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Bwana Mwenyezi-Mungu alinijalia maono mengine: Nilimwona Bwana Mwenyezi-Mungu akiuita moto wa hukumu ya kuwaadhibu watu. Moto huo uliunguza vilindi vikuu vya bahari, ukaanza kuiteketeza nchi kavu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hili ndilo ono, Bwana Mungu alilonionyesha: Nimeona, Bwana Mungu alivyouita moto kuja kumgombea. Nao ukala vilindi vikubwa vya maji, ukataka kula napo pa kulimia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Haya ndiyo aliyonionyesha Bwana MUNGU; tazama, Bwana MUNGU aliita ili kushindana kwa moto; nao ukavila vilindi vikuu, ukataka kuiteketeza nchi kavu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Bwana wetu Yawe alinionyesha tena maono mengine: Bwana wetu Yawe akiuita moto wa hukumu wa kuwaazibu watu. Moto ule uliunguza vilindi vikubwa vya bahari, ukaanza kuiteketeza inchi kavu.