Amos 8:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye Mwenyezi-Mungu akaniuliza: “Amosi, unaona nini?” Nami nikamjibu, “Naona kikapu cha matunda ya kiangazi.” Kisha Mwenyezi-Mungu akaniambia: “Mwisho umewafikia watu wangu wa Israeli. Sitavumilia tena maovu yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akaniuliza, “Amosi, unaona nini?” Nikajibu, “Kikapu chenye matunda yaliyoiva.” Ndipo Mwenyezi Mungu akaniambia, “Wakati umewadia kwa watu wangu Israeli; sitawahurumia zaidi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaniambia, Amosi, unaona nini? Nikasema, Naona kikapu cha matunda ya wakati wa hari. Ndipo Bwana akaniambia, Mwisho wao umewajilia watu wangu Israeli; sitawapita tena kamwe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye Mwenyezi-Mungu akaniuliza: “Amosi, unaona nini?” Nami nikamjibu, “Naona kikapu cha matunda ya kiangazi.” Kisha Mwenyezi-Mungu akaniambia: “Mwisho umewafikia watu wangu wa Israeli. Sitavumilia tena maovu yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akaniuliza, “Amosi, unaona nini?” Nikajibu, “Kikapu chenye matunda yaliyoiva.” Ndipo BWANA akaniambia, “Wakati umewadia kwa watu wangu Israeli, sitawahurumia zaidi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akaniuliza, “Amosi, unaona nini?” Nikajibu, “Kikapu chenye matunda yaliyoiva.” Ndipo bwana akaniambia, “Wakati umewadia kwa watu wangu Israeli; sitawahurumia zaidi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akaniambia, Amosi, unaona nini? Nikasema, Naona kikapu cha matunda ya wakati wa joto. Ndipo BWANA akaniambia, Mwisho wao watu wangu Israeli umewajia; sitawapita tena kamwe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye Mwenyezi-Mungu akaniuliza: “Amosi, unaona nini?” Nami nikamjibu, “Naona kikapu cha matunda ya kiangazi.” Kisha Mwenyezi-Mungu akaniambia: “Mwisho umewafikia watu wangu wa Israeli. Sitavumilia tena maovu yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Unaona nini, Amosi? Niliposema: Kikapu chenye matunda yaliyoiva, Bwana akaniambia: Zimetimia siku za kuishia kwao walio ukoo wangu wa Isiraeli, sitaendelea tena kuwapita tu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaniambia, Amosi, unaona nini? Nikasema, Naona kikapu cha matunda ya wakati wa hari. Ndipo BWANA akaniambia, Mwisho wao umewajilia watu wangu Israeli; sitawapita tena kamwe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye Yawe akaniuliza: Amosi, unaona nini? Nami nikamujibu: Ninaona kikapu cha matunda yenye kuivya. Kisha Yawe akaniambia: Mwisho umewafikia watu wangu wa Israeli. Sitavumilia tena maovu yao.