Amos 9:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nilimwona Mwenyezi-Mungu amesimama kando ya madhabahu, naye akaniamuru: “Zipige hizo nguzo za hekalu mpaka misingi yake itikisike. Zivunje hizo nguzo ziwaangukie watu vichwani. Wale watakaosalia nitawaua kwa upanga; hakuna hata mmoja wao atakayenusurika, naam, hakuna atakayetoroka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nilimwona Bwana akiwa amesimama kando ya madhabahu, naye akasema: “Piga vichwa vya nguzo ili vizingiti vitikisike. Viangushe juu ya vichwa vya watu wote; na wale watakaosalia nitawaua kwa upanga. Hakuna yeyote atakayekimbia, hakuna atakayetoroka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nalimwona Bwana akisimama karibu na madhabahu; akasema, vipigo vichwa vya nguzo, hata vizingiti vitikisike; vivunje vipande vipande juu ya kichwa cha kila mmoja wao; nami nitamwua mtu wa mwisho wao kwa upanga; hapana hata mmoja wao atakayekimbia, wala hataokoka hata mmoja wao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nilimwona Mwenyezi-Mungu amesimama kando ya madhabahu, naye akaniamuru: “Zipige hizo nguzo za hekalu mpaka misingi yake itikisike. Zivunje hizo nguzo ziwaangukie watu vichwani. Wale watakaosalia nitawaua kwa upanga; hakuna hata mmoja wao atakayenusurika, naam, hakuna atakayetoroka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nilimwona Bwana akiwa amesimama kando ya madhabahu, naye akasema: “Piga juu ya nguzo ili vizingiti vitikisike. Viangushe juu ya vichwa vya watu wote, na wale watakaosalia nitawaua kwa upanga. Hakuna awaye yote atakayekimbia, hakuna atakayetoroka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nilimwona Bwana akiwa amesimama kando ya madhabahu, naye akasema: “Piga vichwa vya nguzo ili vizingiti vitikisike. Viangushe juu ya vichwa vya watu wote; na wale watakaosalia nitawaua kwa upanga. Hakuna awaye yote atakayekimbia, hakuna atakayetoroka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nilimwona Bwana akisimama karibu na madhabahu; akasema, Vipige vichwa vya nguzo, hata vizingiti vitikisike; vivunje vipande vipande juu ya kichwa cha kila mmoja wao; nami nitamwua mtu wa mwisho wao kwa upanga; hapana hata mmoja wao atakayekimbia, wala hataokoka hata mmoja wao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nilimwona Mwenyezi-Mungu amesimama kando ya madhabahu, naye akaniamuru: “Zipige hizo nguzo za hekalu mpaka misingi yake itikisike. Zivunje hizo nguzo ziwaangukie watu vichwani. Wale watakaosalia nitawaua kwa upanga; hakuna hata mmoja wao atakayenusurika, naam, hakuna atakayetoroka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nimemwona Bwana, akisimama penye kutambikia na kusema: Zipige nguzo pembeni juu, vizingiti vya juu vitikisike! Kisha uviponde, viwaangukie vichwani pao wote! nao watakaosalia nitawaua kwa upanga, pasiwe hata mmoja kwao, atakayekimbia, wala mmoja wao atakayepona.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nalimwona Bwana akisimama karibu na madhabahu; akasema, vipigo vichwa vya nguzo, hata vizingiti vitikisike; vivunje vipande vipande juu ya kichwa cha kila mmoja wao; nami nitamwua mtu wa mwisho wao kwa upanga; hapana hata mmoja wao atakayekimbia, wala hataokoka hata mmoja wao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nilimwona Yawe akisimama pembeni ya mazabahu, naye akaniamuru: Piga zile nguzo za hekalu mpaka misingi yake itikisike. Uvunje zile nguzo ziwaangukie watu juu ya vichwa. Wale watakaobaki nitawaua kwa upanga; hakuna hata mumoja wao atakayeponyoka, hakuna atakayetoroka.