Amos 9:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Wakati waja kwa hakika, ambapo mara baada ya kulima mavuno yatakuwa tayari kuvunwa; mara baada ya kupanda mizabibu utafuata wakati wa kuvuna zabibu. Milima itabubujika divai mpya, navyo vilima vitatiririka divai.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Siku zinakuja,” asema Mwenyezi Mungu, “wakati mvunaji atatanguliwa na mkulima, naye mpanzi atatanguliwa na yeye akamuaye zabibu. Divai mpya itadondoka kutoka milimani, na kutiririka kutoka vilima vyote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Angalieni, siku zinakuja, asema Bwana, ambazo huyo alimaye atamfikilia avunaye, na yeye akanyagaye zabibu atamfikilia apandaye mbegu; nayo milima itadondoza divai tamu, na vilima vyote vitayeyuka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Wakati waja kwa hakika, ambapo mara baada ya kulima mavuno yatakuwa tayari kuvunwa; mara baada ya kupanda mizabibu utafuata wakati wa kuvuna zabibu. Milima itabubujika divai mpya, navyo vilima vitatiririka divai.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Siku zinakuja,” asema BWANA, “wakati mvunaji atakapotanguliwa na mkulima na mpanzi atakapotanguliwa na yeye akamuaye zabibu. Divai mpya itadondoka kutoka milimani na kutiririka kutoka vilima vyote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Siku zinakuja,” asema bwana, “wakati mvunaji atatanguliwa na mkulima, naye mpanzi atatanguliwa na yeye akamuaye zabibu. Divai mpya itadondoka kutoka milimani, na kutiririka kutoka vilima vyote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Angalieni, siku zinakuja, asema BWANA, ambazo huyo alimaye atamfikia avunaye, na yeye akanyagaye zabibu atamfikia apandaye mbegu; nayo milima itadondoza divai tamu, na vilima vyote vitayeyuka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Wakati waja kwa hakika, ambapo mara baada ya kulima mavuno yatakuwa tayari kuvunwa; mara baada ya kupanda mizabibu utafuata wakati wa kuvuna zabibu. Milima itabubujika divai mpya, navyo vilima vitatiririka divai.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, asemavyo Bwana: Mtaona, siku zikija, mwenye kulima atakaposhikamana na mvunaji, vile vile mwenye kuzikamua zabibu na mpanda mbegu. Ndipo, milima itakapochuruzika pombe mbichi, vilima vyote vifurikwe nazo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Angalieni, siku zinakuja, asema BWANA, ambazo huyo alimaye atamfikilia avunaye, na yeye akanyagaye zabibu atamfikilia apandaye mbegu; nayo milima itadondoza divai tamu, na vilima vyote vitayeyuka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku zinakuja ambapo wakati wa kuvuna utafuata mbio wakati wa kulima, wakati wa kukamua zabibu utafuata mbio wakati wa kupanda mizabibu. –Ni ujumbe wa Yawe.– Milima itabubujika divai mupya, navyo vilima vitatiririka divai.