Amos 9:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitarekebisha hali ya watu wangu Waisraeli. Watajenga miji yao iliyoharibiwa na kuishi humo; watapanda mizabibu na kunywa divai yake; watalima mashamba na kula mazao yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitawarejesha tena watu wangu Israeli waliohamishwa; wataijenga tena miji iliyoachwa magofu, nao wataishi ndani yake. Watapanda mizabibu na kunywa divai yake; watalima bustani na kula matunda yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nitawarejeza tena watu wangu Israeli waliohamishwa, nao wataijenga miji iliyoachwa maganjo, na kukaa ndani yake; nao watapanda mizabibu katika mashamba, na kunywa divai yake; nao watafanyiza bustani, na kula matunda yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitarekebisha hali ya watu wangu Waisraeli. Watajenga miji yao iliyoharibiwa na kuishi humo; watapanda mizabibu na kunywa divai yake; watalima mashamba na kula mazao yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitawarejesha tena watu wangu Israeli waliohamishwa; wataijenga tena miji iliyoachwa magofu, nao wataishi ndani mwake. Watapanda mizabibu na kunywa divai yake, watalima bustani na kula matunda yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitawarejesha tena watu wangu Israeli waliohamishwa; wataijenga tena miji iliyoachwa magofu, nao wataishi ndani mwake. Watapanda mizabibu na kunywa divai yake; watalima bustani na kula matunda yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nitawarejesha tena watu wangu Israeli waliohamishwa, nao wataijenga miji iliyoachwa maganjo, na kukaa ndani yake; nao watapanda mizabibu katika mashamba, na kunywa divai yake; nao watatengeneza bustani, na kula matunda yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nitarekebisha hali ya watu wangu Waisraeli. Watajenga miji yao iliyoharibiwa na kuishi humo; watapanda mizabibu na kunywa divai yake; watalima mashamba na kula mazao yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, nitakapoyafungua mafungo yao walio ukoo wangu wa Isiraeli, waijenge miji yao iliyoangamizwa, waipande mizabibu yao, wapate kunywa mvinyo zao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nitawarejeza tena watu wangu Israeli waliohamishwa, nao wataijenga miji iliyoachwa maganjo, na kukaa ndani yake; nao watapanda mizabibu katika mashamba, na kunywa divai yake; nao watafanyiza bustani, na kula matunda yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitarudisha hali ya mbele ya watu wangu Waisraeli. Watajenga miji yao iliyoharibiwa na kuishi ndani yake; watapanda mizabibu na kunywa divai yake; watalima mashamba na kula mazao yake.