Amos 9:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wajapochukuliwa mateka na adui zao, huko nitatoa amri wauawe kwa upanga. Nitawachunga kwa makini sana niwatendee mabaya na si mema.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wajapopelekwa uhamishoni na adui zao, huko nako nitaamuru upanga uwaue. Nitawakazia macho yangu kwa mabaya wala si kwa mazuri.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao wajapokwenda hali ya kufungwa mbele ya adui zao, nitauagiza upanga huko, nao utawaua; nami nitawaelekezea macho yangu niwatende mabaya, wala si mema.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wajapochukuliwa mateka na adui zao, huko nitatoa amri wauawe kwa upanga. Nitawachunga kwa makini sana niwatendee mabaya na si mema.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wajapopelekwa uhamishoni na adui zao, huko nako nitaamuru upanga uwaue. Nitawakazia macho yangu kwa mabaya wala si kwa mazuri.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wajapopelekwa uhamishoni na adui zao, huko nako nitaamuru upanga uwaue. Nitawakazia macho yangu kwa mabaya wala si kwa mazuri.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao wajapokwenda kuwa mateka mbele ya adui zao, nitauagiza upanga huko, nao utawaua; nami nitawaelekezea macho yangu niwatende mabaya, wala si mema.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wajapochukuliwa mateka na adui zao, huko nitatoa amri wauawe kwa upanga. Nitawachunga kwa makini sana niwatendee mabaya na si mema.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ingawa waje mbele ya adui zao wakihamishwa kwenda utumwani, huko nako nitawaagizia upanga, uwaue; ndipo, nitakapowaelekezea macho yangu, niwapatie mabaya, nisiwapatie mema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao wajapokwenda hali ya kufungwa mbele ya adui zao, nitauagiza upanga huko, nao utawaua; nami nitawaelekezea macho yangu niwatende mabaya, wala si mema.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hata wakikamatwa mateka na waadui zao, nitatoa amri kule wauawe kwa upanga. Nitawachunga kwa uangalifu sana nipate kuwatendea mabaya na si mema.