Amos 9:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Bwana Mwenyezi-Mungu wa majeshi, anaigusa ardhi nayo inatetemeka na wakazi wake wanaomboleza; dunia nzima inapanda na kushuka kama kujaa na kupwa kwa mto Nili wa Misri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, yeye agusaye dunia nayo ikayeyuka, na wote wanaoishi ndani yake wakaomboleza: nayo nchi yote huinuka kama Mto Naili, kisha hushuka kama mto wa Misri;
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana Bwana, MUNGU wa majeshi, ndiye aigusaye nchi, nayo ikayeyuka, na wote wakaao ndani yake wataomboleza; nayo itainuka yote pia kama Mto, nayo itakupwa tena kama Mto wa Misri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Bwana Mwenyezi-Mungu wa majeshi, anaigusa ardhi nayo inatetemeka na wakazi wake wanaomboleza; dunia nzima inapanda na kushuka kama kujaa na kupwa kwa mto Nili wa Misri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Bwana, BWANA Mwenye Nguvu Zote, yeye agusaye dunia nayo ikayeyuka, na wote wakaao ndani mwake wakaomboleza: nayo nchi yote huinuka kama Nile, kisha hushuka kama mto wa Misri;
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Bwana, bwana Mwenye Nguvu Zote, yeye agusaye dunia nayo ikayeyuka, na wote wakaao ndani mwake wakaomboleza: nayo nchi yote huinuka kama Naili, kisha hushuka kama mto wa Misri;
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana Bwana, MUNGU wa majeshi, ndiye aigusaye nchi, nayo ikayeyuka, na wote wakaao ndani yake wataomboleza; nayo itainuka yote pia kama Nili, nayo itakupwa tena kama Mto wa Misri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Bwana Mwenyezi-Mungu wa majeshi, anaigusa ardhi nayo inatetemeka na wakazi wake wanaomboleza; dunia nzima inapanda na kushuka kama kujaa na kupwa kwa mto Nili wa Misri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo, Bwana Mungu Mwenye vikosi atakapoigusa nchi, itayeyuka papo hapo, wote wakaao huko waomboleze; ndipo, nchi yote itakapojitutumua kama mto wa Nili, kisha itakupwa kama lile jito la Misri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana Bwana, MUNGU wa majeshi, ndiye aigusaye nchi, nayo ikayeyuka, na wote wakaao ndani yake wataomboleza; nayo itainuka yote pia kama Mto, nayo itakupwa tena kama Mto wa Misri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Bwana wetu Yawe wa majeshi, anaigusa dunia nayo inatetemeka, na wakaaji wake wanaomboleza; dunia nzima inapanda na kushuka kama vile muto Nili wa Misri unavyojaa na kupunguka.