Amos 9:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu amejenga makao yake mbinguni, nayo dunia akaifunika kwa anga; huyaita maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya nchi kavu. Mwenyezi-Mungu, ndilo jina lake!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
yeye ambaye hujenga jumba lake la kifalme katika mbingu na kuisimika misingi yake juu ya dunia, yeye aitaye maji ya bahari na kuyamwaga juu ya nchi: Mwenyezi Mungu ndilo jina lake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yeye ndiye avijengaye vyumba vyake mbinguni, na kuweka misingi ya kuba yake juu ya nchi; yeye ndiye ayaitaye maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya uso wa nchi; Bwana ndilo jina lake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu amejenga makao yake mbinguni, nayo dunia akaifunika kwa anga; huyaita maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya nchi kavu. Mwenyezi-Mungu, ndilo jina lake!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
yeye ambaye hujenga jumba lake la kifalme katika mbingu na kuisimika misingi yake juu ya dunia, yeye aitaye maji ya bahari na kuyamwaga juu ya uso wa nchi: BWANA ndilo jina lake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
yeye ambaye hujenga jumba lake la kifalme katika mbingu na kuisimika misingi yake juu ya dunia, yeye aitaye maji ya bahari na kuyamwaga juu ya uso wa nchi: bwana ndilo jina lake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yeye ndiye avijengaye vyumba vyake mbinguni, na kuweka misingi ya kuba yake juu ya nchi; yeye ndiye ayaitaye maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya uso wa nchi; BWANA ndilo jina lake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu amejenga makao yake mbinguni, nayo dunia akaifunika kwa anga; huyaita maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya nchi kavu. Mwenyezi-Mungu, ndilo jina lake!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndiye aliyepajenga pake mbinguni kuwa dari yake, nayo misingi ya kao lake aliiweka chini; ndiye anayeyaita maji ya baharini, ayafurikishe juu ya nchi kavu. Bwana ni Jina lake!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yeye ndiye avijengaye vyumba vyake mbinguni, na kuweka misingi ya kuba yake juu ya nchi; yeye ndiye ayaitaye maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya uso wa nchi; BWANA ndilo jina lake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe amejenga makao yake mbinguni, nayo dunia akaifunika kwa anga; anayaita maji ya bahari, na kuyamwanga juu ya inchi kavu. Yawe, ndilo jina lake!