Amos 9:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Kwangu mimi, nyinyi Waisraeli, hamna tofauti yoyote na watu wa Kushi! Niliwatoa Wafilisti kutoka Krete, na Waashuru kutoka Kiri, kama nilivyowatoa nyinyi kutoka Misri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Je, Waisraeli, ninyi si sawa kwangu kama Wakushi?” asema Mwenyezi Mungu. “Je, sikuleta Israeli kutoka Misri, Wafilisti kutoka Kaftori, na Washamu kutoka Kiri?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Je! Ninyi si kama wana wa Wakushi kwangu mimi, enyi wana wa Israeli, asema Bwana? Je! Mimi sikuwapandisha Israeli toka nchi ya Misri, na Wafilisti toka Kaftori, na Washami toka Kiri?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Kwangu mimi, nyinyi Waisraeli, hamna tofauti yoyote na watu wa Kushi! Niliwatoa Wafilisti kutoka Krete, na Waashuru kutoka Kiri, kama nilivyowatoa nyinyi kutoka Misri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Je, Waisraeli, ninyi si sawa kwangu kama Wakushi?” asema BWANA. “Je, sikuleta Israeli kutoka Misri, Wafilisti toka Kaftori na Washami kutoka Kiri?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Je, Waisraeli, ninyi si sawa kwangu kama Wakushi?” asema bwana. “Je, sikuleta Israeli kutoka Misri, Wafilisti kutoka Kaftori, na Washamu kutoka Kiri?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Je! Ninyi si kama wana wa Wakushi kwangu mimi, enyi wana wa Israeli, asema BWANA? Je! Mimi sikuwapandisha Israeli toka nchi ya Misri, na Wafilisti toka Kaftori, na Washami toka Kiri?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Kwangu mimi, nyinyi Waisraeli, hamna tofauti yoyote na watu wa Kushi! Niliwatoa Wafilisti kutoka Krete, na Waashuru kutoka Kiri, kama nilivyowatoa nyinyi kutoka Misri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, yeye Bwana asemavyo: Ham sawasawa kama wana wa Kinubi, ninyi wana wa Isiraeli? Waisiraeli sikuwatoa katika nchi ya Misri? Nao Wafilisti kule Kafutori? Nao Washami kule Kiri?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Je! Ninyi si kama wana wa Wakushi kwangu mimi, enyi wana wa Israeli, asema BWANA? Je! Mimi sikuwapandisha Israeli toka nchi ya Misri, na Wafilisti toka Kaftori, na Washami toka Kiri?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwangu mimi, ninyi Waisraeli, muko sawasawa na watu wa Kushi! –Ni ujumbe wa Yawe.– Niliwatoa Wafilistini kutoka Krete, na Waaramu kutoka Kiri, kama nilivyowatoa ninyi kutoka Misri.