Amos 9:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mimi, Bwana Mwenyezi-Mungu nautazama ufalme wenye dhambi, na nitauangamiza kabisa kutoka duniani. Lakini sitawaangamiza wazawa wote wa Yakobo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Hakika macho ya Bwana Mungu Mwenyezi yako juu ya ufalme wenye dhambi. Nami nitauangamiza kutoka uso wa dunia: hata hivyo sitaiangamiza kabisa nyumba ya Yakobo,” asema Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Angalieni, macho ya Bwana MUNGU yanauangalia ufalme wenye dhambi, nami nitauangamiza utoke juu ya uso wa dunia; lakini sitaiangamiza kabisa nyumba ya Yakobo, asema Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mimi, Bwana Mwenyezi-Mungu nautazama ufalme wenye dhambi, na nitauangamiza kabisa kutoka duniani. Lakini sitawaangamiza wazawa wote wa Yakobo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Hakika macho ya BWANA Mwenyezi yako juu ya ufalme wenye dhambi. Nami nitauangamiza kutoka kwenye uso wa dunia: hata hivyo sitaiangamiza kabisa nyumba ya Yakobo,” asema BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Hakika macho ya bwana Mwenyezi yako juu ya ufalme wenye dhambi. Nami nitauangamiza kutoka kwenye uso wa dunia: hata hivyo sitaiangamiza kabisa nyumba ya Yakobo,” asema bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Angalieni, macho ya Bwana MUNGU yanauangalia ufalme wenye dhambi, nami nitauangamiza utoke juu ya uso wa dunia; lakini sitaiangamiza kabisa nyumba ya Yakobo, asema BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mimi, Bwana Mwenyezi-Mungu nautazama ufalme wenye dhambi, na nitauangamiza kabisa kutoka duniani. Lakini sitawaangamiza wazawa wote wa Yakobo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtaona, macho yangu Bwana Mungu yakiutazama ufalme uliokosa niutoweshe juu ya nchi, lakini sitautowesha mlango wa Yakobo wote mzima; ndivyo, asemavyo Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Angalieni, macho ya Bwana MUNGU yanauangalia ufalme wenye dhambi, nami nitauangamiza utoke juu ya uso wa dunia; lakini sitaiangamiza kabisa nyumba ya Yakobo, asema BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninauangalia ufalme wenye zambi, na nitauangamiza kabisa kutoka katika dunia. Lakini sitawaangamiza wazao wote wa Yakobo. –Ni ujumbe wa Yawe.