Colossians 1:11 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mungu awajalieni nguvu kwa uwezo wake mtukufu ili muweze kustahimili kila kitu kwa uvumilivu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
mkiwa mmetiwa nguvu kwa uwezo wote kwa kadiri ya nguvu yake yenye utukufu, ili mpate kuwa na wingi wa saburi na uvumilivu. Nanyi kwa furaha
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
mkiwezeshwa kwa uwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake, mpate kuwa na saburi ya kila namna na uvumilivu pamoja na furaha;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
ili Mungu mwenyewe awaimarishe kwa uwezo wake mkuu, ili muwe na uvumilivu pasipo kukata tamaa mnapokutana na shida. Ndipo nanyi mtakapofurahi,
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mungu awajalieni nguvu kwa uwezo wake mtukufu ili mweze kustahimili kila kitu kwa uvumilivu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mungu awajalieni nguvu kwa uwezo wake mtukufu ili muweze kustahimili kila kitu kwa uvumilivu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mkiwa mmetiwa nguvu kwa uwezo wote kwa kadiri ya nguvu yake yenye utukufu, ili mpate kuwa na wingi wa saburi na uvumilivu, nanyi kwa furaha
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
mkiwa mmetiwa nguvu kwa uwezo wote kwa kadiri ya nguvu yake yenye utukufu, ili mpate kuwa na wingi wa saburi na uvumilivu. Nanyi kwa furaha
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
mkiwezeshwa kwa uwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake, mpate kuwa na subira ya kila namna na uvumilivu pamoja na furaha;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mungu awajalieni nguvu kwa uwezo wake mtukufu ili muweze kustahimili kila kitu kwa uvumilivu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena tunawaombea, mtiwe nguvu zo zote kwa hivyo, utukufu wake ulivyo wenye nguvu, mpate kuyavumilia na kuyanyenyekea yote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
mkiwezeshwa kwa uwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake, mpate kuwa na saburi ya kila namna na uvumilivu pamoja na furaha;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mungu atawatia nguvu kwa uwezo wake wenye utukufu, kusudi mupate kuvumilia kila kitu pasipo kuchoka. Basi kwa furaha,
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
mkiwezeshwa kwa nwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake, mpate kuwa na saburi ya killa namna na uvumilivu pamoja na furaha;