Colossians 1:17 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yeye alikuwako kabla ya vitu vyote; vyote huendelea kuwako kwa uwezo wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yeye alikuwako kabla ya vitu vyote, na katika yeye vitu vyote vinashikamana pamoja.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mwana alikuwapo kabla ya kuumbwa kitu chochote, na vyote vinaendelea kuwepo kwa sababu yake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kristo alikuwako kabla ya vitu vyote; kwa kuungana naye, vyote vyadumu mahali pake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yeye alikuwako kabla ya vitu vyote; vyote huendelea kuwako kwa uwezo wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yeye alikuwapo kabla ya vitu vyote na katika yeye vitu vyote vinashikamana pamoja.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yeye alikuwepo kabla ya vitu vyote, na katika yeye vitu vyote vinashikamana pamoja.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yeye alikuwako kabla ya vitu vyote; vyote huendelea kuwako kwa uwezo wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye mwenyewe alikuwapo, vitu vyote vilipokuwa havijakuwapo bado, navyo vyote hushikwa naye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kristo alikuwa yuko mbele vitu vyote havijakuwa, na kwa njia ya kuungana naye vyote vinashikamana.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
nae alikuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye.