Colossians 1:18 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yeye ni kichwa cha mwili wake, yaani kanisa; yeye ni chanzo cha uhai wa huo mwili. Yeye ndiye mwanzo, mzaliwa wa kwanza aliyefufuliwa kutoka kwa wafu, ili awe na nafasi ya kwanza katika vitu vyote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yeye ndiye kichwa cha mwili, yaani jumuiya ya waumini, naye ndiye mwanzo na mzaliwa wa kwanza kutoka kwa wafu, ili yeye awe mkuu katika vitu vyote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yeye ni kichwa cha mwili, yaani kanisa. Yeye ni mwanzo wa maisha yajayo, ni wa kwanza miongoni mwa wote watakaofufuliwa kutoka kwa wafu. Hivyo katika mambo yote yeye ni mkuu zaidi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yeye ni kichwa cha mwili wake, yaani kanisa; yeye ni chanzo cha uhai wa huo mwili. Yeye ndiye mwanzo, mzaliwa wa kwanza aliyefufuliwa kutoka wafu, ili awe na nafasi ya kwanza katika vitu vyote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yeye ni kichwa cha mwili wake, yaani kanisa; yeye ni chanzo cha uhai wa huo mwili. Yeye ndiye mwanzo, mzaliwa wa kwanza aliyefufuliwa kutoka kwa wafu, ili awe na nafasi ya kwanza katika vitu vyote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yeye ndiye kichwa cha mwili, yaani, Kanisa, naye ni wa mwanzo na mzaliwa wa kwanza kutoka kwa wafu, ili yeye awe mkuu katika vitu vyote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yeye ndiye kichwa cha mwili, yaani jumuiya ya waumini, naye ndiye mwanzo na mzaliwa wa kwanza kutoka kwa wafu, ili yeye awe mkuu katika vitu vyote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yeye ni kichwa cha mwili wake, yaani kanisa; yeye ni chanzo cha uhai wa huo mwili. Yeye ndiye mwanzo, mzaliwa wa kwanza aliyefufuliwa kutoka kwa wafu, ili awe na nafasi ya kwanza katika vitu vyote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye mwenyewe ni kichwa cha mwili, maana cha wateule. Naye ni wa kwanza, ni limbuko la wafu, kusudi yeye awe wa kwanza katika mambo yote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yeye ni kichwa cha kanisa linalokuwa mwili wake. Naye ndiye asili ya uzima wa mwili ule. Yeye ndiye mwanzo, muzaliwa wa kwanza, na ndiye aliyefufuka wa kwanza, kusudi akuwe wa kwanza juu ya vyote.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nae ni kichwa cha mwili, yaani cha kanisa; nae ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, illi awe mtangulizi katika yote.