Colossians 1:2 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
tunawaandikia nyinyi watu wa Mungu huko Kolosai, ndugu zetu waaminifu katika kuungana na Kristo. Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa ndugu watakatifu na waaminifu katika Al-Masihi wanaoishi Kolosai. Neema na amani zinazotoka kwa Mungu, Baba yetu, ziwe nanyi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kwa ndugu watakatifu, waaminifu katika Kristo, walioko Kolosai. Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Salamu kwenu kaka na dada zetu watakatifu na walio waaminifu katika Kristo mlioko Kolosai. Neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu ziwe pamoja nanyi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
tunawaandikia ninyi watu wa Mungu huko Kolosai, ndugu zetu waaminifu katika kuungana na Kristo. Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
tunawaandikia nyinyi watu wa Mungu huko Kolosai, ndugu zetu waaminifu katika kuungana na Kristo. Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa ndugu watakatifu na waaminifu katika Kristo, waishio Kolosai: Neema iwe nanyi na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa ndugu watakatifu na waaminifu katika Al-Masihi, waishio Kolosai: Neema na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu ziwe nanyi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kwa ndugu watakatifu na waaminifu katika Kristo, walioko Kolosai. Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
tunawaandikia nyinyi watu wa Mungu huko Kolosai, ndugu zetu waaminifu katika kuungana na Kristo. Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
tunawaandikia ninyi mlioko Kolose, ndugu watakatifu mnaomtegemea Kristo: Upole uwakalie na utengemano unaotoka kwa Mungu Baba yetu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kwa ndugu watakatifu, waaminifu katika Kristo, walioko Kolosai. Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tunawaandikia ninyi watu wa Mungu munaokaa katika muji Kolosayi, ninyi wandugu munaoungana na Kristo kwa uaminifu. Tunawatakia neema na amani toka kwa Mungu Baba yetu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
kwa ndugu watakatifu na waaminifu, walio ndani ya Kolossai, Neema iwe kwenu na imani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.