Colossians 1:22 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini sasa, kwa kifo cha Mwanae aliyeishi hapa duniani, Mungu amewapatanisha naye, kusudi awaweke mbele yake mkiwa watakatifu, safi na bila lawama.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini sasa Mungu amewapatanisha ninyi kupitia kwa mwili wa Al-Masihi kupitia mauti, ili awalete mbele zake mkiwa watakatifu, bila dosari wala lawama,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
katika mwili wa nyama yake, kwa kufa kwake, ili awalete ninyi mbele zake, watakatifu, wasio na mawaa wala lawama;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini sasa amewafanya kuwa marafiki zake tena, kupitia kifo cha Kristo katika mwili wake. Ili kwa njia hiyo awalete kwake mkiwa watakatifu, msio na lawama na msiohukumiwa jambo lolote mbele zake;
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini sasa, kwa kifo cha Mwanae aliyeishi hapa duniani, Mungu amewapatanisha naye, kusudi awalete mbele yake mkiwa watakatifu, safi na bila lawama.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini sasa, kwa kifo cha Mwanae aliyeishi hapa duniani, Mungu amewapatanisha naye, kusudi awaweke mbele yake mkiwa watakatifu, safi na bila lawama.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini sasa Mungu amewapatanisha ninyi kwa njia ya mwili wa Kristo kwa kupitia mauti, ili awalete mbele zake mkiwa watakatifu, bila dosari wala lawama,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini sasa Mungu amewapatanisha ninyi kwa njia ya mwili wa Al-Masihi kupitia mauti, ili awalete mbele zake mkiwa watakatifu, bila dosari wala lawama,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
katika mwili wa nyama yake, kwa kufa kwake, ili awalete ninyi mbele zake, watakatifu, wasio na mawaa wala lawama;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini sasa, kwa kifo cha Mwanae aliyeishi hapa duniani, Mungu amewapatanisha naye, kusudi awaweke mbele yake mkiwa watakatifu, safi na bila lawama.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini sasa amewapatanisha hata ninyi hapo, alipokufa na kuutoa mwili wake wa kimtu, awageuze nanyi kuwa machoni pake watakatifu pasipo kilema wala kosa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
katika mwili wa nyama yake, kwa kufa kwake, ili awalete ninyi mbele zake, watakatifu, wasio na mawaa wala lawama;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sasa, Mungu amewapatanisha ninyi naye, kwa njia ya kufa kwa Mwana wake kimwili, kusudi awawezeshe kuonekana mbele yake mukiwa watakatifu, bila kilema wala kosa lolote.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
katika mwili wa nyama yake, kwa kufa kwake, illi awalete ninyi mbele zake, watakatifu, hamna mawaa wala lawama,