Colossians 1:23 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mnapaswa, lakini kuendelea na msingi imara katika imani, wala msikubali kutikiswa kutoka katika tumaini lile mlilopata wakati mlipoisikia Injili. Mimi Paulo nimekuwa mtumishi wa hiyo Injili ambayo imekwisha hubiriwa kila mtu duniani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
ikiwa mnaendelea katika imani yenu mkiwa imara na thabiti, pasipo kuliacha tumaini lililoahidiwa katika Injili. Hii ndiyo ile Injili mliyoisikia, ambayo imehubiriwa kwa kila kiumbe chini ya mbingu, na ambayo mimi Paulo nimekuwa mtumwa wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
mkidumu tu katika ile imani, hali mmewekwa juu ya msingi, mkawa imara; msipogeuzwa na kuliacha tumaini la Injili mliyosikia habari zake, iliyohubiriwa katika viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu; ambayo mimi Paulo nalikuwa mhudumu wake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
na hiki ndicho kitatokea mkiendelea kuiamini Habari Njema mliyoisikia. Mwendelee kuwa imara na kudumu katika imani. Jambo lolote lisiwafanye mkaliacha tumaini lenu mlilopokea mlipoisikia Habari Njema. Habari Njema ile ile ambayo imehubiriwa kwa kila mtu duniani, ndiyo kazi ambayo mimi, Paulo, nilipewa kufanya.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mnapaswa, lakini kuendelea kuwa imara na thabiti katika imani hiyo, na msikubali kusukumwa mbali na tumaini lile mlilopata wakati mlipoisikia Habari Njema. Mimi Paulo nimekuwa mtumishi wa hiyo Habari Njema ambayo imekwisha hubiriwa kila kiumbe duniani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mnapaswa, lakini kuendelea na msingi imara katika imani, wala msikubali kutikiswa kutoka katika tumaini lile mlilopata wakati mlipoisikia Injili. Mimi Paulo nimekuwa mtumishi wa hiyo Injili ambayo imekwisha hubiriwa kila mtu duniani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
mradi tu kwamba mnaendelea kuwa waaminifu, mkiwa mmefanywa imara na thabiti katika imani, pasipo kuliacha tumaini lililoahidiwa na Injili. Hii ndiyo ile Injili mliyoisikia ambayo imehubiriwa kwa kila kiumbe chini ya mbingu na ambayo mimi Paulo, nimekuwa mtumwa wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
ikiwa mnaendelea katika imani yenu mkiwa imara na thabiti, pasipo kuliacha tumaini lililoahidiwa katika Injili. Hii ndiyo ile Injili mliyoisikia, ambayo imehubiriwa kwa kila kiumbe chini ya mbingu, na ambayo mimi Paulo nimekuwa mtumwa wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
mkidumu tu katika ile imani, hali mmewekwa juu ya msingi, mkawa imara; msipogeuzwa na kuliacha tumaini la Injili mliyosikia habari zake, iliyohubiriwa kwa viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu; ambayo mimi Paulo nilikuwa mhudumu wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mnapaswa, lakini kuendelea na msingi imara katika imani, wala msikubali kutikiswa kutoka katika tumaini lile mlilopata wakati mlipoisikia Injili. Mimi Paulo nimekuwa mtumishi wa hiyo Injili ambayo imekwisha hubiriwa kila mtu duniani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtakuwa hivyo mkifuliza kumtegemea, kwani mmajengwa juu ya msingi wenye nguvu, msiwezekane kuondolewa penye kingojeo cha Utume mwema, mliousikia; ndio unaotangaziwa kila kiumbe kilichoko chini ya mbingu. Nami Paulo ninautumikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
mkidumu tu katika ile imani, hali mmewekwa juu ya msingi, mkawa imara; msipogeuzwa na kuliacha tumaini la Injili mliyosikia habari zake, iliyohubiriwa katika viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu; ambayo mimi Paulo nalikuwa mhudumu wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini, inawapasa ninyi kuendelea na musingi imara katika imani, musitikiswe na kupoteza lile tumaini mulilopata wakati muliposikia Habari Njema. Mimi Paulo nimewekwa kuwa mutumishi wa kuhubiri Habari Njema ile iliyokwisha kutangazwa kwa watu wote katika dunia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
mkidumu tu katika imani, mmewekwa juu ya misingi, mkawa imara; msipogeuzwa na kuliacha tumaini la Injili mliyosikia khabari zake, iliyokhubiriwa katika viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu; ambayo mimi Paolo nalikuwa mkhudumu wake.