Colossians 1:7 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mlijifunza juu ya neema ya Mungu kutoka kwa Epafra, mtumishi mwenzetu, ambaye ni mfanyakazi mwaminifu wa Kristo kwa niaba yetu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mlijifunza habari zake kutoka kwa Epafra, mtumishi mwenzetu mpendwa, aliye mhudumu mwaminifu wa Al-Masihi kwa ajili yenu,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kama mlivyofundishwa na Epafra, mjoli wetu mpenzi, aliye mhudumu mwaminifu wa Kristo kwa ajili yenu;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kweli hiyo mliisikia kutoka kwa Epafra, aliye mtumwa wa Bwana pamoja nasi. Yeye anatusaidia sisi kama mtumishi mwaminifu wa Kristo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mlijifunza juu ya neema ya Mungu kutoka kwa Epafra, mtumishi mwenzetu, ambaye ni mfanyakazi mwaminifu wa Kristo kwa niaba yetu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mlijifunza juu ya neema ya Mungu kutoka kwa Epafra, mtumishi mwenzetu, ambaye ni mfanyakazi mwaminifu wa Kristo kwa niaba yetu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mlijifunza habari zake kutoka kwa Epafra, mtumishi mwenzetu mpendwa, yeye aliye mhudumu mwaminifu wa Kristo kwa ajili yenu,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mlijifunza habari zake kutoka kwa Epafra, mtumishi mwenzetu mpendwa, yeye aliye mhudumu mwaminifu wa Al-Masihi kwa ajili yenu,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kama mlivyofundishwa na Epafra, mwenzi wetu mpendwa, aliye mhudumu mwaminifu wa Kristo kwa ajili yenu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mlijifunza juu ya neema ya Mungu kutoka kwa Epafra, mtumishi mwenzetu, ambaye ni mfanyakazi mwaminifu wa Kristo kwa niaba yetu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, mlivyofundishwa na Epafura; ni mtumwa mwenzetu mpendwa, tena ni mtumishi mwelekevu wa Kristo anayewafanyizia ninyi kazi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kama mlivyofundishwa na Epafra, mjoli wetu mpenzi, aliye mhudumu mwaminifu wa Kristo kwa ajili yenu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ni Epafra mutumishi mwenzetu mupenzi, ndiye aliyewafundisha ninyi habari zile. Yeye ni mutumishi mwaminifu wa Kristo kwa ajili yetu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
kama mlivyofundishwa na Epafra mjoli wetu mpenzi, aliye mkhudumu amini wa Kristo kwa ajili yenu;