Colossians 2:1 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Napenda mjue jinsi ninavyofanya kazi kwa bidii kwa ajili yenu, kwa ajili ya watu wa Laodikea na kwa ajili ya wote ambao hawajapata kuniona kwa macho.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nataka mjue jinsi ninavyojitaabisha kwa ajili yenu na kwa ajili ya wale walio Laodikia, na pia kwa ajili ya wote ambao hawajapata kuniona mimi binafsi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana nataka ninyi mjue jinsi ilivyo kuu juhudi yangu niliyo nayo kwa ajili yenu, na kwa ajili ya wale wa Laodikia, na wale wasioniona uso wangu katika mwili;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ninataka mfahamu ni kwa kiwango gani ninawajali ninyi pamoja na ndugu waishio Laodikia na wengine ambao hawajawahi kuniona.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Napenda mjue jinsi ninavyofanya kazi kwa bidii kwa ajili yenu, kwa ajili ya watu wa Laodikea na kwa ajili ya wote ambao hawajapata kuniona kwa macho.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Napenda mjue jinsi ninavyofanya kazi kwa bidii kwa ajili yenu, kwa ajili ya watu wa Laodikea na kwa ajili ya wote ambao hawajapata kuniona kwa macho.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa nataka mjue jinsi ninavyojitaabisha kwa ajili yenu na kwa ajili ya wale walioko Laodikia na kwa ajili ya wote wale ambao hawajapata kuniona mimi binafsi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nataka mjue jinsi ninavyojitaabisha kwa ajili yenu na kwa ajili ya wale walioko Laodikia, na pia kwa ajili ya wote ambao hawajapata kuniona mimi binafsi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana nataka ninyi mjue jinsi ilivyo kuu juhudi yangu niliyo nayo kwa ajili yenu, na kwa ajili ya wale wa Laodikia, na wale wasioniona uso wangu katika mwili;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Napenda mjue jinsi ninavyofanya kazi kwa bidii kwa ajili yenu, kwa ajili ya watu wa Laodikea na kwa ajili ya wote ambao hawajapata kuniona kwa macho.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani nataka, mlijue shindano langu kubwa, nililo nalo kwa ajili yenu na ya Walaodikia na kwa ajili yao wote wasioniona uso kwa uso kimwili; nalo ni hili:
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana nataka ninyi mjue jinsi ilivyo kuu juhudi yangu niliyo nayo kwa ajili yenu, na kwa ajili ya wale wa Laodikia, na wale wasioniona uso wangu katika mwili;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninataka mujue jinsi ninavyofanya kazi kwa bidii kwa ajili yenu, kwa ajili ya waamini wa Laodikia na kwa ajili ya wote ambao hawajapata kuniona bado.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
MAANA nataka muijue juhudi niliyo nayo kwa ajili yenu, na kwa ajili ya wale wa Laodikia, na wale wasioniona uso wangu katika mwili, jinsi ilivyo kuu;