Colossians 2:11 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Katika kuungana na Kristo nyinyi mlitahiriwa, lakini si kwa tohara ifanywayo na watu, bali inayofanywa na Kristo mwenyewe, na ambayo inahusikana na kukombolewa kutoka katika utu wa dhambi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika Al-Masihi pia mlitahiriwa kwa kutengwa mbali na asili ya dhambi, si kwa tohara inayofanywa kwa mikono ya wanadamu, bali kwa ile tohara iliyofanywa na Al-Masihi,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Katika yeye mmetahiriwa kwa tohara isiyofanyika kwa mikono, kwa kuuvua mwili wa nyama, kwa tohara ya Kristo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mlitahiriwa katika Kristo kwa namna tofauti, si kwa mikono ya kibinadamu. Hii ni kusema ya kwamba, mlishiriki katika kifo cha Kristo, ambacho kilikuwa aina ya tohara kwa namna ya kuuvua mwili wake wa kibinadamu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Katika kuungana na Kristo ninyi mlitahiriwa, lakini si kwa tohara ifanywayo na watu, bali inayofanywa na Kristo mwenyewe, na ambayo inahusikana na kukombolewa kutoka katika utu wa dhambi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Katika kuungana na Kristo nyinyi mlitahiriwa, lakini si kwa tohara ifanywayo na watu, bali inayofanywa na Kristo mwenyewe, na ambayo inahusikana na kukombolewa kutoka katika utu wa dhambi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika Kristo pia mlitahiriwa kwa kutengwa mbali na asili ya dhambi, si kwa tohara inayofanywa kwa mikono ya wanadamu bali kwa ile tohara iliyofanywa na Kristo,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika Al-Masihi pia mlitahiriwa kwa kutengwa mbali na asili ya dhambi, si kwa tohara inayofanywa kwa mikono ya wanadamu, bali kwa ile tohara iliyofanywa na Al-Masihi,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Katika yeye mmetahiriwa kwa tohara isiyofanyika kwa mikono, kwa kuuvua mwili wa nyama, kwa tohara ya Kristo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Katika kuungana na Kristo nyinyi mlitahiriwa, lakini si kwa tohara ifanywayo na watu, bali inayofanywa na Kristo mwenyewe, na ambayo inahusikana na kukombolewa kutoka katika utu wa dhambi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena mkiwa naye yeye hutahiriwa pasipo kutumia mikono ya mtu, maana huuvua mwili wa kimtu ulio wenye makosa, ndiko kutahiriwa Kikristo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Katika yeye mmetahiriwa kwa tohara isiyofanyika kwa mikono, kwa kuuvua mwili wa nyama, kwa tohara ya Kristo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika kuungana naye, mumetahiriwa wala si kwa mikono ya watu, lakini mumetahiriwa na Kristo, na kutahiriwa kule kumewakomboa toka katika hali zaifu ya kimwili.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Katika yeye mmetahiriwa kwa tohara isiyofanyika kwa mkono, kwa kuuvua mwili wa dhambi, wa nyama, kwa tohara ya Kristo;