Colossians 2:12 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana, mlipobatizwa mlizikwa pamoja na Kristo, na katika ubatizo mlifufuliwa pia pamoja naye kwa kuamini katika nguvu ya Mungu ambaye alimfufua Kristo kutoka kwa wafu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
mkiwa mmezikwa pamoja naye katika ubatizo, na kufufuliwa pamoja naye kupitia kwa imani yenu katika uweza wa Mungu, aliyemfufua kutoka kwa wafu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mkazikwa pamoja naye katika ubatizo; na katika huo mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na mlipobatizwa, mlizikwa na kufufuka pamoja naye kutokana na imani yenu kwa nguvu za Mungu aliyemfufua Kristo kutoka katika kifo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana, mlipobatizwa mlizikwa pamoja na Kristo, na katika ubatizo, mlifufuliwa pia pamoja naye kwa imani yenu katika nguvu ya Mungu ambaye alimfufua Kristo kutoka wafu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana, mlipobatizwa mlizikwa pamoja na Kristo, na katika ubatizo mlifufuliwa pia pamoja naye kwa kuamini katika nguvu ya Mungu ambaye alimfufua Kristo kutoka kwa wafu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
mkiwa mmezikwa pamoja naye katika ubatizo na kufufuliwa pamoja naye kwa njia ya imani yenu katika uweza wa Mungu aliyemfufua kutoka kwa wafu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
mkiwa mmezikwa pamoja naye katika ubatizo, na kufufuliwa pamoja naye kwa njia ya imani yenu katika uweza wa Mungu, aliyemfufua kutoka kwa wafu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mkazikwa pamoja naye katika ubatizo; na katika huo mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana, mlipobatizwa mlizikwa pamoja na Kristo, na katika ubatizo mlifufuliwa pia pamoja naye kwa kuamini katika nguvu ya Mungu ambaye alimfufua Kristo kutoka kwa wafu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo, mlipobatizwa mmezikwa pamoja naye, tena papo hapo mmefufuliwa pamoja naye kwa nguvu ya kumtegemea, mwipatayo kwake, Mungu aliyemfufua katika wafu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mkazikwa pamoja naye katika ubatizo; na katika huo mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana mumezikwa pamoja na Kristo kwa njia ya ubatizo, nanyi mumefufuliwa vilevile pamoja naye, kwa sababu mumeamini uwezo wa Mungu, aliyemufufua.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
mkizikwa pamoja nae katikti ubatizo, katika huo mlifufuliwa pamoja nae, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu.