Colossians 2:14 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
alifutilia mbali ile hati ya deni iliyokuwa inatukabili na masharti yake, na kuifuta kabisa kwa kuipigilia msalabani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
baada ya kuifuta ile hati yenye mashtaka yaliyokuwa yanatukabili, pamoja na maagizo yake. Aliiondoa isiwepo tena, akaigongelea kwenye msalaba wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa sababu tulizivunja sheria za Mungu, tunalo deni. Kumbukumbu ya deni hilo imeorodhesha amri zote tulizoshindwa kuzifuata. Lakini Mungu ametusamehe deni hilo. Ameiondoa kumbukumbu yake na kuipigilia msalabani.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
alifutilia mbali ile hati ya deni iliyokuwa inatukabili na masharti yake, na kuifuta kabisa kwa kuipigilia msalabani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
alifutilia mbali ile hati ya deni iliyokuwa inatukabili na masharti yake, na kuifuta kabisa kwa kuipigilia msalabani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
akiisha kuifuta ile hati yenye mashtaka yaliyokuwa yanatukabili pamoja na amri zake, aliiondoa isiwepo tena, akiigongomea kwenye msalaba wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
akiisha kuifuta ile hati yenye mashtaka yaliyokuwa yanatukabili, pamoja na maagizo yake. Aliiondoa isiwepo tena, akiigongomea kwenye msalaba wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
alifutilia mbali ile hati ya deni iliyokuwa inatukabili na masharti yake, na kuifuta kabisa kwa kuipigilia msalabani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akakifuta cheti kilichoandikwa maagizo, tusiyoyashika, ndicho kilichotusuta; akakiondoa hapo kati, akakipigilia msalabani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alifuta barua ya madeni yetu na sherti zilizotushitaki. Aliyafuta kabisa kwa kuyapigilia juu ya musalaba.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
akiisba kuifuta ile khati iliyoandikwa na kutushitaki kwa hukumu zake; iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwe kati kati yetu sisi na yeye, akaikaza msalabani;