Colossians 2:15 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huko Kristo aliwapokonya nguvu zao hao pepo watawala na wakuu; aliwafanya kuwa kitu cha fedheha hadharani kwa kuwaburuta kama mateka katika msafara wa ushindi wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya Mungu kuzivua enzi na mamlaka, aliziaibisha hadharani, akishangilia katika ushindi wa msalaba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Pale msalabani, aliwanyang'anya watawala wa ulimwengu wa roho nguvu na mamlaka. Aliwashinda pale. Na akawafukuza kama wafungwa ili ulimwengu wote uone.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Juu ya msalaba Kristo aliwapokonya nguvu zao hao pepo watawala na wakuu; aliwafanya kuwa kitu cha fedheha hadharani kwa kuwaburuta kama mateka katika msafara wa ushindi wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Huko Kristo aliwapokonya nguvu zao hao pepo watawala na wakuu; aliwafanya kuwa kitu cha fedheha hadharani kwa kuwaburuta kama mateka katika msafara wa ushindi wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mungu akiisha kuzivua enzi na mamlaka, alizifanya kuwa kitu cha fedheha hadharani kwa kuziburura kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba wa Kristo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mungu akiisha kuzivua enzi na mamlaka, alizifanya kuwa kitu cha fedheha hadharani kwa kuziburura kwa ujasiri, akizishinda katika msalaba wa Al-Masihi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuziaibisha hadharani, akiziongoza kwa ushindi wake wa shangwe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Huko Kristo aliwapokonya nguvu zao hao pepo watawala na wakuu; aliwafanya kuwa kitu cha fedheha hadharani kwa kuwaburuta kama mateka katika msafara wa ushindi wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao wakuu wa wangavu akawavua ukuu wao na nguvu zao, akaonyesha waziwazi, walivyo, akawatembeza kama mateka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mungu alinyanganya uwezo wa wakubwa na wenye mamlaka, naye akawaonyesha waziwazi, akiwatembeza kama wafungwa katika maandamano ya ushindi wa Mwana wake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
akiisha kuziteka enzi na mamlaka, na kuzimithilisha kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo.