Colossians 2:19 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
na amejitenga na Kristo aliye kichwa cha huo mwili. Chini ya uongozi wa Kristo, mwili wote unalishwa na kuunganishwa pamoja kwa viungo na mishipa yake, nao hukua kama atakavyo Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yeye amepoteza ushirikiano na Kichwa, ambaye kutoka kwake mwili wote unalishwa na kushikamanishwa pamoja kwa viungo na mishipa, nao hukua jinsi Mungu anavyouwezesha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wala hakishiki Kichwa, ambacho kwa yeye mwili wote ukiruzukiwa na kuungamanishwa kwa viungo na mishipa, hukua kwa maongeo yatokayo kwa Mungu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hawajafungamanishwa na kichwa; Kristo ndiye kichwa, na mwili wote humtegemea Yeye. Kwa sababu ya Kristo viungo vyote vya mwili vinatunzana na kusaidiana kila kimoja na kingine. Hivyo mwili hupata nguvu zaidi na kufungamana pamoja kadri Mungu anavyouwezesha kukua.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
na amejitenga na Kristo aliye kichwa cha huo mwili. Chini ya uongozi wa Kristo, mwili wote unalishwa na kuunganishwa pamoja kwa viungo na mishipa yake, nao hukua kama atakavyo Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
na amejitenga na Kristo aliye kichwa cha huo mwili. Chini ya uongozi wa Kristo, mwili wote unalishwa na kuunganishwa pamoja kwa viungo na mishipa yake, nao hukua kama atakavyo Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
wala hakishiki kwa uthabiti kichwa, ambaye kutoka kwake mwili wote unalishwa na kushikamanishwa pamoja kwa viungo na mishipa, ambao hukua kwa ukuaji utokao kwa Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yeye amepoteza ushirikiano na Kichwa, ambaye kutoka kwake mwili wote unalishwa na kushikamanishwa pamoja kwa viungo na mishipa, nao hukua kwa ukuaji utokao kwa Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
wala hakishiki Kichwa, ambacho kwa yeye mwili wote ukineemeshwa na kuungamanishwa kwa viungo na mishipa, hukua kama atakavyo Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
na amejitenga na Kristo aliye kichwa cha huo mwili. Chini ya uongozi wa Kristo, mwili wote unalishwa na kuunganishwa pamoja kwa viungo na mishipa yake, nao hukua kama atakavyo Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
asishikamane naye aliye kichwa, aliye mwenye kuuunganisha mwili wote, ukitiwa nguvu kwa fundo na viungo, upate kumkulia Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wala hakishiki Kichwa, ambacho kwa yeye mwili wote ukiruzukiwa na kuungamanishwa kwa viungo na mishipa, hukua kwa maongeo yatokayo kwa Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutu yule hashikamani na Kristo anayekuwa kichwa cha mwili. Chini ya uongozi wa Kristo, mwili muzima unakulishwa vizuri na kuunganishwa pamoja kwa njia ya maunganio na vifundo vyake, kusudi upate kukomaa kufuatana na mapenzi ya Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
wala hakishiki kiehwa, ambacho kwa yeye mwili wote ukiruzukiwa na kuungamanishwa kwa viungo na mishipa, hukua mkuo utokao kwa Mungu.