Colossians 2:20 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nyinyi mmekufa pamoja na Kristo na kukombolewa katika nguvu za pepo watawala wa ulimwengu. Kwa nini, basi, kuishi tena kama vile mngekuwa wa ulimwengu huu? Ya nini kuwekewa masharti:
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa mlikufa pamoja na Al-Masihi, mkayaacha yale mafundisho ya msingi ya ulimwengu huu, kwa nini bado mnaishi kana kwamba ninyi ni wa ulimwengu? Kwa nini mnajitia chini ya amri kama hizi:
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi ikiwa mlikufa pamoja na Kristo mkayaacha yale mafundisho ya awali ya ulimwengu, kwa nini kujitia chini ya amri, kama wenye kuishi duniani,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mlikufa pamoja na Kristo na kuwekwa huru kutoka katika nguvu zinazotawala dunia. Hivyo kwa nini mnaishi kama watu ambao bado mngali wa ulimwengu? Nina maana kuwa, kwa nini mnafuata sheria hizi:
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ninyi mmekufa pamoja na Kristo na kukombolewa kutoka nguvu za pepo watawala wa ulimwengu. Kwa nini, basi, kuishi tena kama vile mngekuwa wa ulimwengu huu? Ya nini kuwekewa masharti:
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nyinyi mmekufa pamoja na Kristo na kukombolewa katika nguvu za pepo watawala wa ulimwengu. Kwa nini, basi, kuishi tena kama vile mngekuwa wa ulimwengu huu? Ya nini kuwekewa masharti:
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa mlikufa pamoja na Kristo, mkayaacha yale mafundisho ya msingi ya ulimwengu huu, kwa nini bado mnaishi kama vile ninyi ni wa ulimwengu? Kwa nini mnajitia chini ya amri:
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa mlikufa pamoja na Al-Masihi, mkayaacha yale mafundisho ya msingi ya ulimwengu huu, kwa nini bado mnaishi kama ninyi ni wa ulimwengu? Kwa nini mnajitia chini ya amri:
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi ikiwa mlikufa pamoja na Kristo mkayaacha yale mafundisho ya awali ya ulimwengu, kwa nini kujitia chini ya amri, kama wenye kuishi duniani,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nyinyi mmekufa pamoja na Kristo na kukombolewa katika nguvu za pepo watawala wa ulimwengu. Kwa nini, basi, kuishi tena kama vile mngekuwa wa ulimwengu huu? Ya nini kuwekewa masharti:
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama mmekufa pamoja naye Kristo mkiyaacha yale mambo yaliyo ya kwanza humu ulimwenguni, kwa nini mwataka tena kupewa miiko kama wenye kuukalia ulimwengu huu?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi ikiwa mlikufa pamoja na Kristo mkayaacha yale mafundisho ya awali ya ulimwengu, kwa nini kujitia chini ya amri, kama wenye kuishi duniani,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninyi mumekufa pamoja na Kristo na kukombolewa toka katika uwezo wa roho mbaya zinazotawala dunia. Kwa nini munaishi tena kama watu wa dunia mukilazimishwa kushika kanuni kama hizi:
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi ikiwa mlikufa pamoja na Kristo mkaacha mafundisho ya awali ya ulimwengu, ya nini kujitia chini ya amri, kama wenye kuishi duniani,