Colossians 2:22 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mambo hayo yote yanahusika na vitu vyenye kuharibika mara tu vinapotumiwa; hayo ni maagizo na mafundisho ya kibinadamu tu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Amri hizi zote mwisho wake ni kuharibika zinapotumiwa, kwa sababu msingi wake ni katika maagizo na mafundisho ya wanadamu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
(mambo hayo yote huharibika wakati wa kutumiwa); hali mkifuata maagizo na mafundisho ya wanadamu?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Sheria hizi zinazungumzia vitu vya kidunia, vitu vinavyotokomea baada ya kutumiwa. Ni amri na mafundisho ya kibinadamu tu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mambo hayo yote yanahusika na vitu vyenye kuharibika mara tu vinapotumiwa; hayo ni maagizo na mafundisho ya kibinadamu tu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mambo hayo yote yanahusika na vitu vyenye kuharibika mara tu vinapotumiwa; hayo ni maagizo na mafundisho ya kibinadamu tu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Haya yote mwisho wake ni kuharibika yanapotumiwa, kwa sababu huo msingi wake ni katika maagizo na mafundisho ya wanadamu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Haya yote mwisho wake ni kuharibika yanapotumiwa, kwa sababu msingi wake ni katika maagizo na mafundisho ya wanadamu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
(mambo hayo yote huharibika wakati wa kutumiwa); hali mkifuata maagizo na mafundisho ya wanadamu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mambo hayo yote yanahusika na vitu vyenye kuharibika mara tu vinapotumiwa; hayo ni maagizo na mafundisho ya kibinadamu tu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Navyo vyote vimewekwa, vitumike, kisha vioze. Kwa hiyo yale maagizo na mafundisho ni ya kimtu tu;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
(mambo hayo yote huharibika wakati wa kutumiwa); hali mkifuata maagizo na mafundisho ya wanadamu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mambo hayo yote yanaelekea vitu vyenye kuharibika mara moja tu vinapotumiwa. Navyo vyote ni kanuni na mafundisho ya watu tu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
(Mambo hayo yote huharibika wakati wa kutumiwa), mkifuata maagizo na mafundislio ya wana Adamu?