Colossians 2:5 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana, ingawa mimi niko mbali nanyi kwa mwili, lakini niko pamoja nanyi kwa roho, na ninafurahi kuona uthabiti kamili mnaosimama nao pamoja katika imani yenu kwa Kristo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa ingawa mimi siko pamoja nanyi kimwili, niko pamoja nanyi kiroho, nami nafurahi kuuona utaratibu wenu na jinsi uthabiti wa imani yenu katika Al-Masihi ulivyo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana nijapokuwa sipo kwa mwili, lakini nipo pamoja nanyi kwa roho, nikifurahi na kuuona utaratibu wenu na uthabiti wa imani yenu katika Kristo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ingawa niko mbali kimwili, niko pamoja nanyi katika roho. Ninafurahi kuona jinsi mnavyofanya kazi vizuri pamoja na jinsi imani yenu ilivyo thabiti katika Kristo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana, ingawa mimi niko mbali nanyi kwa mwili, lakini niko pamoja nanyi kwa roho, na ninafurahi kuona uthabiti kamili mnaosimama nao pamoja katika imani yenu kwa Kristo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana, ingawa mimi niko mbali nanyi kwa mwili, lakini niko pamoja nanyi kwa roho, na ninafurahi kuona uthabiti kamili mnaosimama nao pamoja katika imani yenu kwa Kristo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana ingawa mimi siko pamoja nanyi kimwili, lakini niko pamoja nanyi kiroho, nami nafurahi kuuona utaratibu wenu na jinsi gani uthabiti wa imani yenu katika Kristo ulivyo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa ingawa mimi siko pamoja nanyi kimwili, lakini niko pamoja nanyi kiroho, nami nafurahi kuuona utaratibu wenu na jinsi uthabiti wa imani yenu katika Al-Masihi ulivyo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana nijapokuwa sipo kwa mwili, lakini nipo pamoja nanyi kwa roho, nikifurahi na kuuona utaratibu wenu na uthabiti wa imani yenu katika Kristo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana, ingawa mimi niko mbali nanyi kwa mwili, lakini niko pamoja nanyi kwa roho, na ninafurahi kuona uthabiti kamili mnaosimama nao pamoja katika imani yenu kwa Kristo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani mwili ukiwa hauko kwenu, moyo uko pamoja nanyi, ukaning'aa ukiona, mwonyekavyo, tena mjishupazavyo kumtegemea Kristo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana nijapokuwa sipo kwa mwili, lakini nipo pamoja nanyi kwa roho, nikifurahi na kuuona utaratibu wenu na uthabiti wa imani yenu katika Kristo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ijapokuwa mimi ni mbali nanyi kwa mwili, lakini mimi ni pamoja nanyi kwa roho, nami ninafurahi kuona namna munavyoishi katika utaratibu muzuri na kusimama imara katika imani mbele ya Kristo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana nijapokuwa sipo kwa mwili, illakini nipo pamoja nanyi kwa roho, nikifurahi na kuuona utaratibu wenu na uthabiti wa imani yenu katika Kristo.