Colossians 2:7 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Muwe na mizizi ndani yake, mjijenge juu yake na kuwa imara katika imani kama mlivyofundishwa. Muwe na shukrani tele.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
mkijikita na kujengwa ndani yake, mkiimarishwa katika imani kama mlivyofundishwa, na kufurika kwa wingi wa shukrani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wenye shina na wenye kujengwa katika yeye; mmefanywa imara kwa imani, kama mlivyofundishwa; mkizidi kutoa shukrani.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na mizizi yenu ikue hata ndani ya Kristo, na maisha yenu yajengwe juu yake. Kama mlivyofundishwa imani ya kweli mwendelee kuwa imara katika ufahamu wenu katika hilo. Na msiache kumshukuru Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mnapaswa kuwa na mizizi ndani yake, kujijenga juu yake na kuwa imara katika imani yenu kama mlivyofundishwa. Muwe na shukrani tele.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Muwe na mizizi ndani yake, mjijenge juu yake na kuwa imara katika imani kama mlivyofundishwa. Muwe na shukrani tele.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
mwe na mizizi, mkiwa mmejengwa ndani yake, mkiimarishwa katika imani kama mlivyofundishwa na kufurika kwa wingi wa shukrani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
mkiwa na mizizi, na mmejengwa ndani yake, mkiimarishwa katika imani kama mlivyofundishwa, na kufurika kwa wingi wa shukrani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
wenye shina na wenye kujengwa katika yeye; mmefanywa imara kwa imani, kama mlivyofundishwa; mkizidi kutoa shukrani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Muwe na mizizi ndani yake, mjijenge juu yake na kuwa imara katika imani kama mlivyofundishwa. Muwe na shukrani tele.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
mkishusha mizizi mumo humo mwake, mkajengwa mlemle na kuongezwa nguvu za kumtegemea, kama mlivyofundishwa; hivyo mtayavumisha yale mema, mliyogawiwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wenye shina na wenye kujengwa katika yeye; mmefanywa imara kwa imani, kama mlivyofundishwa; mkizidi kutoa shukrani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mukuwe na mizizi ndani yake, mujijenge juu yake na kusimama imara katika imani sawa vile mulivyofundishwa. Na zaidi ya hii mukuwe wenye kushukuru sana.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
mmetia mizizi, na kujengwa katika yeye: mmefanywa imara kwa imani, kaina mlivyofundishwa, mkizidi kutoa shukrani.