Colossians 2:9 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana, ndani yake Kristo katika ubinadamu wake, umo ukamilifu wote wa Mungu,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Maana utimilifu wote wa Mungu unakaa ndani ya Al-Masihi katika umbile la mwili wa kibinadamu,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nasema hili kwa sababu Mungu mwenyewe kama alivyo, ukamilifu wa uungu wake unaishi ndani ya Kristo. Hii ni hata wakati wa maisha yake hapa duniani.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana, ndani yake Kristo katika ubinadamu wake, umo ukamilifu wote wa Mungu,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana, ndani yake Kristo katika ubinadamu wake, umo ukamilifu wote wa Mungu,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Maana ukamilifu wote wa Uungu umo ndani ya Kristo katika umbile la mwili wa kibinadamu,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Maana ukamilifu wote wa Uungu umo ndani ya Al-Masihi katika umbile la mwili wa kibinadamu,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana, ndani yake Kristo katika ubinadamu wake, umo ukamilifu wote wa Mungu,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani mwake Kristo ndimo mkaamo kimwili wingi wao yote yaliyo ya Kimungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana ukamilifu wote wa Mungu uko ndani ya Kristo katika mwili wake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa namna ya kimwili.