Colossians 3:12 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nyinyi ni watu wake Mungu; yeye aliwapenda na kuwateua. Kwa hiyo, basi, vaeni moyo wa huruma, wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi, kwa kuwa ninyi mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wanaopendwa sana, jivikeni moyo wa huruma, utu wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mungu amewachagua na kuwafanya ninyi kuwa watu wake walio watakatifu. Anawapenda. Hivyo, jivikeni matendo haya na muwe na huruma: wema, wanyenyekevu, wapole na wenye subira.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ninyi ni watu wake Mungu; yeye aliwapenda na kuwateua. Kwa hiyo basi, vaeni moyo wa huruma, wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nyinyi ni watu wake Mungu; yeye aliwapenda na kuwateua. Kwa hiyo, basi, vaeni moyo wa huruma, wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo, kwa kuwa ninyi mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu, wapendwao sana, jivikeni moyo wa huruma, utu wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo, kwa kuwa ninyi mmekuwa wateule wa Mwenyezi Mungu, watakatifu wapendwao sana, jivikeni moyo wa huruma, utu wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nyinyi ni watu wake Mungu; yeye aliwapenda na kuwateua. Kwa hiyo, basi, vaeni moyo wa huruma, wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Ninyi watakatifu na wapendwa, kwa hivyo, mlivyochaguliwa na Mungu, vaeni mioyo yenye huruma za kweli na utu na unyenyekevu na upole na uvumilivu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninyi ni watu wa Mungu, yeye amewapenda na kuwachagua kwa ajili yake mwenyewe. Kwa hiyo, mukuwe na moyo wa huruma, wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi, kwa kuwa mu wateule wa Mungu, watakatifu na wapendwao, vaeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu,